Kuhuisha kumbukumbu ya kufariki kwa Ummul Banina (a.s): Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya majlisi ya maombolezo kwa watumishi wake..

Sehemu ya majlisi ya maombolezo
Miongoni mwa ratiba za kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha mama yake Abulfadhil Abbasi (a.s) bibi mtukufu mnusuruji wa kizazi kitakasifu Ummul Banina (a.s) ambaye tupo katika siku za huzuni ya kifo chake, Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya huzuni katika ukumbi wa utawala ndani ya haram tukufu kwa wafanya kazi wake, asubuhi ya Juma Pili (13 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (12 Machi 2017 m).

Majlisi ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na muhadhiri mwenyewe Shekh Muhammad Kuraitwi kutoka katika kitengo cha dini, halafu akazungumza kuhusu maisha ya mama huyu mtukufu, ambaye Mwenyezi Mungu amempa daraja kubwa, amemfanya kua miongoni mwa milango ya rehema zake katika kukidhi shida za watu na kutatua matatizo yao, kwa nini asifanye hivyo wakati mama huyu (a.s) aliwapa kipawa mbele zaidi watoto wa mtume (s.a.w.w) kuliko watoto wake, akajitolea watoto wake waende kumnusuru imamu na ndugu yao Abuu Abdillahi Hussein (a.s) hadi wapate shahada kwa ajili ya kuutetea ujumbe wa Mwenyezi Mungu, ukiongeza sifa zingine nzuri alizo kua nazo mama huyu mtukufu (a.s), mwisho wa majlisi hii zilisomwa qaswida za huzuni kuhusu kufariki kwa mama huyu mtukufu.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalumu kuhusu kuhuisha mnasaba huu wenye kuumiza, wa kukumbuka kufariki kwake (a.s), ratiba hiyo imehusisha vitu vingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: