Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wafanya taazia kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kukumbuka kufariki kwa mama yake Ummul Banina (a.s)..

Maoni katika picha
Bibi mtukufu Ummul Banina (a.s) ana nafasi kubwa sana kwa Ahlulbait (a.s), alikua na ikhlasi kubwa kwa imamu Hussein (a.s), aliwasisitiza wanae watukufu wamhami na kumlinda ndugu yao imamu Hussein (a.s), ni wachache sana watu wa mfano wake, alikua mwana jihadi alijitolea hali na mali kwa ajili ya uislamu.

Tupo katika siku za kukumbuka kufariki kwake tarehe kumi na tatu Jamadil Aakhira, wapenzi wake duniani kote wana huisha kumbu kumbu ya kifo chake, na katika mji wa Karbala na Ataba zake tukufu pia wanahuisha mnasaba huu tene ukizingatia kua Karbala ndio mji mkuu wa huzuni duniani na sehemu walipo uawa watoto wa Ummul Banina (a.s), walipo uawa waja wema walio muhami imamu Hussein (a.s) kwa nafsi zao.

Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wamempa pole kipenzi cha Ummul Banina na tulizo la macho yake Abulfadhil Abbasi (a.s), hakika yeye ndiye mwenye kupewa pole katika tukio hili, vikao nya taazia vilianza kufanyika katika Ataba mbili tukufu ya imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu walipanga mstari wakitanguliwa na katibu wao mkuu pamoja na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na wakuu wa vitengo, ikasomwa ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na wimbo wa Ataba (wa Ibaa), kisha zikasomwa qaswida za huzuni zilizo muhusu Ummul Banina (a.s), kabla hawaja maliza waliingia watumishi wa Atabatu Husseiniyya wakiwa pamoja na katibu wao mkuu na jopo la viongozi ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kua wamefanya majlisi rasmi katika Atabatu Husseiniyya wakaja kuungana na wenzao ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), walipokewa kwa qaswida za huzuni kisha wakasimama pamoja na kuendelea kuimba mashairi ya kuomboleza yaliyo elezea kwa kina utukufu wa mama huyu mtakasifu (a.s), walikhitimisha kwa kusoma maneno ya ahadi ya kuendelea kua waaminifu katika utumishi wao katika hizi sehemu takasifu.

Riwaya nyingi zinasema kua, Ummul Banina (a.s) alifariki tarehe kumi na tatu Jamadil Aakhira, na alizikwa katika makaburi wa Baqii karibu na Ibrahim, Zainabu, Ummu Kulthum, Abdullahi, Qassim na wengineo miongoni mwa maswahaba na mashahidi, kaburi lake lilivunjwa na manawaasibu (matakfiri) pamoja na makaburi ya maimamu wa nyumba ya mtume, imamu Hassan Al-mujtaba, imamu Ali bun Hussein Zainul-abideen, imamu Muhammad bun Ali Al-baaqir na imamu Jafari bun Muhammad Swaadiq (a.s).

Amani imuendee mama mwema mtakasifu, mtekelezaji mwenye ikhlasi, uliye fata nyayo za mbora wa wanawake wa ulimwenguni bibi Fatuma Zaharaa (a.s) katika kutii sheria na mwenendo wa maisha, pongezi kubwa zimuendee yeye na kila atakaye iga mwenendo wake miongoni mwa wanawake wema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: