Hospitali ya rufaa Alkafeel yachukua jukumu la kutibu wairaq walio jeruhiwa katika shambulio la kigaidi lililo tokea Damaska..

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa ya Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa misaada yake ya kibinadamu na kutokana na maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa kiongozi wake mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) imechukua jukumu la kutibu wairaq walio jeruhiwa katika shambulio la kigaidi lililo tokea mji mkuu wa Sirya Damaska.

Mkuu wa hospitali Dokta Haidari Bahadeli alisema kua: “Baada ya agizo la uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, uongozi wa hospitali ya rufaa Alkafeel umejipanga kutoa tiba kwa majeruhi, hadi sasa tumesha pokea watu 37 na tumeandaa timu maalumu ya madaktari wa ndani na nje ya Iraq wanao simamia matubabu yao, matibabu yote yanafanyika bure”.

Akaongeza kusema kua: “Tumepokea majeruhi wa aina mbalimbali, baada ya kuwafanyia uchunguzi wa awali tumekuta kuna walio vinjika viungo na wenye majeraha ya ndani pia wapo tulio wafanyia upasuaji”.

Kumbuka kua siku ya Juma Mosi ilitokea miripuko miwili karibu na makaburi ya Mlango Mdogo (Babu swaghir) katika kitongoji cha Babu Mustwafa mtaa wa Shaghuur ndani ya mji wa Damaska wa zamani, kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Iraq, wananchi wa Iraq walio kufa ni 40 na majeruhi 120 waliokua wameenda kufanya ziara katika malalo matukufu yaliyopo huko.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: