Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu wafika Mosul kutembelea vikosi vya wapiganaji..

Maoni katika picha
Kutokana na umuhimu wa kudumisha mawasiliano na vikosi vya wapikanaji ikiwa kama ni wajibu upande wa kidini na ki-akhlaq hadi kuhakikisha Iraq imewamaliza kabisa magaidi, Atabatu Abbasiyya tukufu bado inaendelea na ratiba yake ya kutembelea vikosi vya wapiganaji waliopo katika uwanja wa vita tangu ilipo tolewa fatwa tukufu na Marjaa dini mkuu hadi leo, kwa ajili ya kuwasaidia kimaanawiyya na kimadiyya.

Ziara ya mwisho ni ile iliyo ongozwa na raisi msaidizi wa kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu Shekh A’adil Wakil pamoja na jopo la Masayyid na Mashekhe watukufu pamoja na baadhi ya watumishi wa Ataba, walitembelea vikosi vya jeshi la serikali na hashdi sha’abi waliopo katika vita vya kuukomboa mji wa Mosul.

Shesk A’adil Wakil alisema kua: “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ugeni huu umeelekea kwa wapiganaji waliopo katika mstari wa mbele katika vita ya kuukomboa mji wa Nainawa, kama mnavyo ona vita kali inaendelea, jambo tunalo weza kufanya ni kuwatembelea na kuwaunga mkono majemedari wetu, hakika wao wapo katika utukufu mkubwa, ziara hii na ziara zingine zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu zinalenga kujenga ari kwa wapiganaji wetu, kwa hakika tumewakuta wakiwa na hamasa ya hali ya juu kabisa, pamoja na kuwapa msaada wa kilojistik kwa vikosi vyote vya hashdi sha’abi, wapiganaji tulio wakuta katika msitari wa mbele kwa hakika wanaimani kubwa, wanaipenda nchi yao na dini yao, wanamsimamo imara sana na ujasiri wa hali ya juu kabisa wako tayari kumtokomeza maluuni daesh, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuonyeshe nusra hivi karibuni na awadhalilishe maadui zetu na maadui wa taifa hili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu hili wingu baya litaondoka katika anga ya Iraq yetu kipenzi”.

Pembezoni mwa ziara hiyo kilifanyika kikao kilicho husisha viongozi wa usalama, akiwemo waziri wa ulinzi wa Iraq Arfani Hayali na kiongozi mkuu wa oporesheni hii ya (Tunakuja ewe Nainawa) Rashidi Yarallah pamoja na kiongozi wa kikosi cha kupambana na ugaidi Abdulghina Asadiy, na kamanda wa kikosi cha Nukhba Mu’an Sa’adiy, ugeni uliangalia maendeleo ya vita na mafanikio yaliyo fikiwa, wakasifu sana juhudi zinazo fanywa na vikosi vwa wapiganaji wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi hususan kufatia ushindi ulio patikana hivi karibuni dhidi ya magaidi ya Daesh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: