Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni Ruhu Nubuwwah yatangaza matokeo ya shindano la kitafiti lililo fanyika..

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni Ruhu Nubuwwah lililo fanywa na shule za Alkafeel za wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Zaharaa –a.s- ni hazina ya elimu na kilele cha hekima) imetangaza matokeo ya shindano la kitafiti yaliyo fanywa katika kongamano hilo, yaliyo husu maisha ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Shekh Amaar Hilali rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu alisema kua: “Hakika kamati ya maandalizi ilifanya mashindano mengi, miongoni mwake ni shindano la kitafiti lililo husisha mada zifuatazo:

  1. Athari za bibi Zaharaa (a.s) kiaqida na kifiqhi.
  2. Upande wa ubinadamu na mfano mkuu katika sira ya Zaharaa (a.s).
  3. Msimamo wa bibi Zaharaa (a.s) katika kutetea haki na maeneo matukufu.
  4. Njia za kurekebisha familia kupitia fikra ya bibi Zaharaa (a.s).
  5. Mazungumzo ya Swidiqa Zaharaa (a.s) katika turathi za uislamu.

Watafiti walio shiriki shindano hili walifika mia moja kumi na tano, na wote walikidhi vigezo vya kielimu na kanuni zilizo wekwa, matokeo yalikua kama ifuatavyo:

Washindi wa nafasi ya kwanza ni mtafiti Twayyiba Ibrahim Abdallah, kupitia utafiti wake usemao: (Mifano bora ya maisha ya ndoa katika sira ya Fatuma Zaharaa –a.s-), na mukarara wa kwanza ni Ustadh Saji Jaasim Muhammad na dokta Anwari Majidi Sarhani, kupitia utafiti wao usemao: (Hotuba ya mwanamke na athari yake.. hotuba ya bibi Zaharaa (a.s) kama mfano).

Washindi wa nafasi ya pili ni dokta Fatuma Karim, kupitia utafiti wake usemao: (Sera ya malezi katika hotuba ya Zaharaa (a.s) ya kuelekeza umma), na wa pili ni mtafiti dokta Zaha Haamid kupitia utafiti wake usemao: (Pande la mtume (s.a.w.w) ni kigezo kwa wanawake na wanaume.. uchambuzi yakinifu), na mukarara wa pili ni wa watafiti wawili, Susan Kadhim Mahdi na Shaimaa Kadhim Mahdi kupitia utafiti wao usemao: (Msimamo wa kiongozi wa umma na malezi ya Muhammadiyya).

Washindi wa nafasi ya tatu ni dokta Zaharaa Nurudini Qaasim, kupitia utafiti wake usemao: (Nyumba ya bibi Fatuma (a.s) ni mwanga wa ukamilifu katika mwenendo wa familia), na mkarara wa tatu ni watafiti Shaima Ni’imah Muhammad na Zainabu Hussein Alwaan, kupitia utafiti wao usemao (upande wa kibinadamu katika hotuba ya bibi Fatuma Zaharaa (a,s) kuhusu Fadaki, dalili za kitafiti kwa lugha ya kiingereza).

Walitangazwa washindi bora zaidi watatu wa mwanzo katika mashindano ya kongamano hili kama ifuatavyo:

Mshindi bora zaidi katika uchoraji wa picha ni Sira Naafii, na mshindi wa ubora wa uwasilishaji ni Amal Ghishawi pamoja na Imani Jafari, na washindi bora zaidi katika hati ni Israa Hamidi na Afafu Zaharaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: