Uhudhuriaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa mjini Bagdadi..

Maoni katika picha
Kutokana na ushiriki wake katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo endelea sasa hivi katika mji mkuu wa Bagdadi, Atabatu Abbasiyya kama kawaida yake imepata muitikio mkubwa kupitia vitengo vyake vinavyo shiriki, ambavyo ni; kitengo cha habari na utamaduni na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, wanaonyesha machapisho yao ambayo yameandikwa na wataalamu wa vitengo hiyo, vitenge hivyo hushirikiana bega kwa bega katika shughuli zao, katika maonyesho haya zinashiriki taasisi na vituo vya usambazaji wa vitabu za kiarabu na kimataifa zipatazo (181) na yataendelea hadi tarehe moja mwezi wa nne 2017 miladia, chini ya kauli mbiu isemayo (Bagdad inasoma).

Ushiriki huu ni miongoni mwa ushiriki mwingi ambao vitengo vya Atabatu Abbasiyya hushiriki, haiishii katika ushiriki peke yake, bali ni nafasi nzuri ya kuielezea Ataba tukufu katika nyanja ya elimu, tamaduni, viwanda, biashara na maendeleo iliyo nayo katika kila sekta, huyafanya maonyesho hayo kama balozi wake, pia hupata fursa ya kuangalia maendeleo ya taasisi zingine za kitaifa na kimataifa, tofauti ya vitengo vya Ataba na vingine ni kwamba, kila kinacho onyeshwa na Ataba ni zao lake halisi, kuanzia utunzi hadi uchapaji.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha hudhuria mara nyingi maonyesho ya vitabu ya kimataifa ambayo hufanywa Bagdad, na huyachukulia kua maonyesho muhimu kwake, pamoja na maonyesho au makongamano mengine ambayo hufanywa ndani au nje ya Iraq yanayo endana na sera yake ambayo ni kueneza fikra na mafundisho ya Ahlulbait (a.s) vitengo vyake hupata muitikio mkubwa kutoka kwa watembeleaji (wadau) na hujitahidi kuongeza bidhaa mpya katika kila maonyesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: