Kumalizika kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwa na kamati ya maandalizi yataka kupanuliwa wigo wa ushiriki..

Maoni katika picha
Alasiri ya siku ya Juma Mosi (26 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (25 Machi 2017 m) ilihitimishwa ratiba ya kongamano la Ruhu Nubuwa lililo simamiwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Zaharaa (a.s) ni hazina ya elimu na kilele cha hekima) lililo dumu kwa siku tatu, ndani ya ukumbi mkuu wa kituo cha Swidiqa Twahira cha harakati za wanawake ambacho kipo chini ya Ataba tukufu katika mji wa Karbala, lilipata muitikio mkubwa kutoka kwa watafiti na wasomi wa sekula wa ndani na nje ya Iraq pamoja na watumishi na wanafunzi wa shule za Alkafeel hali kadhalika wawakilishi wa Ataba za Iraq.

Hafla ilihudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) pamoja na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) na jopo la viongozi wengine, ilifunguliwa kwa kusomwa Qur’an tukufu halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq kisha ukaimbwa mwimbo wa Atabatu Abbasiyya.

Ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) baada ya kuwashukuru na kuwapongeza waumini na Marjaa dini kwa mnasaba huu (kuzaliwa kwa bibi Fatuma –a.s-) alisema kua: “Hakika kongamano hili lina nafasi maalumu katika nyoyo za waumini kutokana na nafasi kubwa aliyo nayo bibi Zaharaa (a.s), tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliye wawezesha waandaaji na washiriki wa kongamano hili tukufu, pia tunamshukuru kwa kutuwezesha kua miongoni mwa wenye kuhuisha uzawa wa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) mtu ambaye hauwezi kuelezea utukufu wake ukaumaliza”.

Kisha Sayyid Ashiqar akaelekeza maneno yake kwa familia za mashahidi, walio poteza uhai kwa ajili ya kulinda aridhi ya nchi hii, akasema: “Amekua kwenu mtume wa Mwenyezi Mungu ni kiigizo chema, na bibi Zaharaa na mwanae bibi Zainabu (a.s) na maimamu wa Ahlulbait (a.s) ni kiigizo chema, walipoteza vipenzi wao kwa ajili ya kupigania dini na walijitolea kila kitu kwa ajili ya dini, kwa dhati ya roho zenu ilipo tolewa fatwa tukufu ya kujilinda mmejitoa na kupigana na maadui wa Mwenyezi Mungu na sunna za mtume wake mmejitolea kwa hali na mali kwa ajili ya lengo hilo tukufu”.

Akamalizia kwa kusema kua: “Tunamshukuru kila aliye changia kufanikisha kwa kongamano hili, na shukrani za pekee nazielekeza kwa kina dada walio andaa na kusimamia kongamano hili tukufu ambalo tunatarajia kulifanya kila mwaka, pia tunawashukuru wageni wetu wote mlio vumilia tabu za safari mkaja kushiriki na kuchangia ufanikishaji wa kongamano hili, ukizingatia limepata watafiti wa kike walio andika kwa kalamu zao mia moja na kumi na tano, hakika idadi hii sio ya kudharau, kuna jambo muhimu sana ambalo limeamshwa kwa kongamano hili, nalo ni kuamsha kalamu za watafiti wa kike pamoja na harakati zingine, kama vile; Qur’an, mashairi, maonyesho na harakati za watoto”.

Ratiba ilihitimishwa kwa kuwapa zawatu washiriki walio shinda katika mashindano yaliyo andaliwa na kongamano hili, ikiwa ni pamoja na mashindano ya kitafiti, Qur’an, mashairi pamoja na kutoa zawadi kwa washiriki wengine.

Kamati ya maangalizi ya kongamano hili wameahidi kufanyika kwa kungamano hili kila mwaka, na kuongeza wigo wa ushiriki zaidi, pia wameahidi kuanzisha jarida la wanawake wa kiislamu litakalo jikita katika kuelezea fikra za bibi Zaharaa (a.s) pia wanatarajia kutengeneza mtandao maalumu wa wanawake wa kiislamu na kuchapisha tafiti zilizo kubalika katika jarida hilo kwa jina la (Tafiti za kongamano la Ruhu Nubuwa) pamoja na kusisitiza kueneza mtazamo wa bibi Zaharaa (a.s) katika jamii ya kiislamu, pamoja na umuhimu wa kuingiza matukufu ya Zaharaa (a.s) katika selebasi za masomo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: