Inafanyika sasa hivi: Kuanza kwa wiki ya kongamano la kitamaduni huko Pakistani (Nasimu Karbala)..

Maoni katika picha
Kabla ya muda mfupi limeanza kongamano katika mji mkuu wa Pakistani Islamabadi, saa kumi alasiri ya leo Juma Tano (30 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (29 Machi 2017) kwa nyakati za Pakistani, wiki ya kitamaduni awamu ya nne (Nasimu Karbala), inasimamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Al-kauthar cha Pakistani, katika kongamano hili zinashiriki (Atabatu Alawiyya, Askariyya na Abbasiyya).

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na msomaji wa Atabatu Alawiyya, Sayyid Hussein Hakeem, katika hafla hii pia ataongea muwakilishi wa Marjaa dini mkuu wa Pakistani, ambae ndiye kiongozi mkuu wa chuo cha Al-kauthar muheshimiwa Shekh Muhsin Ali Najafi, na ujumbe wa kiongozi wa kisheria wa Atabatu Husseiniyya tukufu muheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalaiy utasomwa kwa niaba yake na muwakilishi wake katika kongamano hili Shekh Ali Qar-a’awiy.

Hafla itakua na ratiba ndefu, ikiwemo kupandisha bendera za Ataba tukufu, na ufunguzi wa maonyesho ya vitu vinavyo zalishwa na Ataba hizo.

Tutakujulisheni zaidi kuhusu ratiba ya siku ya kwanza ya wiki hii baada ya saa chache zijazo –inshallah- unaweza kufatilia kinacho endelea kupitia mtandao wetu rasmi wa Alkafeel wa kimataifa katika ukurasa wa face book.

Fahamu kua hafla ilianza saa kumi alasiri kwa majira ya mji mkuu wa Pakistani Islamabad sawa na saa nane adhuhuri kwa majira ya mji mkuu wa Iraq Bagdad.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: