Kutembelea chuo cha wasichana Al-kauthar na hafla za Qur’an ni ratiba muhimu katika siku ya tatu ya wiki ya kitamaduni (Nasimu Karbala) huko Pakistani..

Maoni katika picha
Ratiba muhimu ya leo Ijumaa (02 Rajabu 1438 h) sawa na (31 Machi 2017 m) ambayo ni siku ya tatu ya wiki ya kitamaduni (Nasimu Karbala) awamu ya nne, inayo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu wakishirikiana na chuo cha Al-kauthar cha Pakistani na kushiriki Ataba tukufu za Alawiyya, Askariyya na Abbasiyya ni kutembelea chuo cha wasichana Al-kauthar.

Kulikua na hafla ya kuwapokea wageni kutoka katika Ataba tukufu ambayo ilifunguliwa kwa Qur’an iliyo somwa na msomaji wa Atabatu Alawiyya Sayyid Hussein Hakeem, baada yake ulifuata ujumbe wa Atabatu Husseiniyya tukufu, ulio wasilishwa na Shekh Uzaam Rabii, aliongelea umuhimu wa elimu na kusoma, akasema: “Inatakiwa elimu iwe pamoja na imani na uchamungu, bali inatakiwa imani iitangulie elimu, ili elimu iwe na munufaa kwa watu na isilete madhara, kwa bahati mbaya historia ya wanadamu imejaa matatizo mengi yaliyo pelekea kuuliwa watu wema na wachamungu walio shikamana na dini yao kutokana na matumizi mabaya ya elimu”.

Kisha lilifuatia neno la kushukuru kutoka wa wageni watukufu lililo tolewa na Shekh Abdul-jabbaar Mahmadaawi, ambaye alishukuru mapokezi mazuri waliyo pewa na akasisitiza umuhimu wa kufuata nyayo za bibi Zaharaa (a.s) kwani msingi wa jamii ni familia na msingi wa familia ni mama.

Na jioni ya leo ilifanyika hafla ya Qur’an ambayo walishiriki wasomaji wa kimataifa wa Pakistani ambao ni: Najmu Mustafa Swaahibu na Haafidh Aakasha Haidari Baaqiriy, na Hussein Swaahibu pamoja na msomaji wa Atabatu Alawiyya tukufu Sayyid Hussein Hakeem na wa Atabatu Askariyya Swadiqu Zaidiy, hafla hii ilifanyika kutokana na imani kua Qur’an humea katika nyoyo za watu wenye imani, hivyo inatakiwa kufundishwa kwa wana jamii ili kurekebisha nyoyo zao, na kuhakikisha wanapambika na tabia za Qur’an, hili haliwezi kufanikiwa kama hakuna ushirikiano wa karibu na kufanyika kwa hafla kama hizi, pamoja na makongamano ya kitaifa na kimataifa yenye ratiba tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: