Atabatu Askariyya tukufu: Zaidi ya watu milioni mbili wamefanya ziara katika kumbukumbu ya shahada ya imamu Haadi (a.s)..

Maoni katika picha
Atabatu Askariyya tukufu imetangaza kukamilika kwa msimu wa ziara za kuhuisha kumbukumbu ya shahada ya imamu Haadi (a.s) ambayo imedumu kwa siku tatu kuanzia siku ya kwanza ya mwezi wa Rajabu Aswabu hadi leo siku ya tatu, idadi ya watu waliokuja kufanya ziara ndani ya siku hizo tatu imefika milioni mbili kutoka katika mikoa mbalimbali ya Iraq na katika nchi za kiislamu.

Atabatu Askariyya tukufu iliweka ratiba kamili ya ulinzi wa amani na utoaji wa huduma kwa kushirikiana na vikosi vya usalama vya Samara na viongozi wa Hashdi Sha’abi, wanajeshi walijipanga barabara yote inayo onganisha Bagdad na mji wa Samara na pembezoni mwa mji wa zamani.

Hali kadhalika, vitengo vya Ataba tukufu viliwasiliana na Ataba zingine, wakfu shia, mazaru za kishia na wizara ya usafirishaji, biashara, mafuta pamoja na viongozi wa mkoa wa Bagdad na wizara ya afya na vituo vya kutoa huduma katika mji wa Samara ili kuhakikisha swala hili linapata ufanisi mkubwa.

Pia vikundi na mawaakibu za Husseiniyya ambazo zilifika (200) zilikua na nafasi kubwa katika kutoa huduma ya chakula, pamoja na mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Askariyya tukufu ambayo imetoa zaidi ya milo elfu sabini (70,000) ya chakula kwa mazuwaru watukufu, vilevile waandishi wa habari walikua na nafasi kubwa sana ya kurusha matukio ya ziara, kulikua na zaidi ya vyombo vya habari vya tv (20) vikiwemo vitano vilivyo tumia magari kurusha matangazo ya moja kwa moja.

Atabatu Askariyya tukufu inatoa shukrani sana kwa kila aliye shiriki na kuchangia mafanikio ya ziara hii tukufu iliyo hudhuriwa na mamilioni ya watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: