Zaidi ya watu (100) wanaume na wanawake wamehitimu kozi ya kujenga uwezo ya tatu kuhusu kuandika tafiti za Qur’an kwa kufuata mwenendo wa vizito viwili..

Maoni katika picha
Watu zaidi ya (100) wamehitimu kozi ya kujenga uwezo ya tatu yenye anuani ya: (Vipi utaandika utafiti kuhusu Qur’an kwa mwenendo wa vizito viwili) iliyo endeshwa na kituo cha maarifa ya Qur’an na kuifasiri na kuichapisha chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mtandao wa Alkafeel ulikutana na muheshimiwa Shekh Dhiyaau Dini Zubaidiy mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur’an na kuifasiri na kuichapisha aliye kua mkufunzi na msimamizi wa semina hiyo, alisema kua: “Semina iliyo andaliwa na kuendeshwa na tawi la Maahadi ya Qur’an tukufu katika mji wa Sha’abu ndani ya mji mkuu wa Bagdad, ilikua semina muhimu sana, ilikua na washiriki zaidi ya (100) wa kiume na wakike wakiwemo wasomi wa sekula kutoka vyuo vikuu tofauti, wakiwemo wasomi (wajawid) wa Qur’an, watafiti na walimu wa Qur’an tukufu, walihudhuria kuongeza ujuzi wao katika semina iliyo dumu wiki nzima.

Akafafanua kua: “Washiriki wamefundishwa historia ya Qur’an tukufu, elimu zake, visomo vyake na riwaya za Ahlulbait (a.s) pamoja na njia za kuzifikia, na namna ya kunufaika na hazina hii muhimu katika kufanya tafiti za kielimu kuhusu Qur’an ukizingatia kua ndio misingi madhubuti alio sema Mtume (s..a.w.w) kupitia hadithi ya Thaqalaini ambayo ni mutawatir (imepokewa na maswahaba wengi)”.

Akasisitiza kua: “Sisi tutaendelea kufanya semina kama hii kutokana na ratiba yetu ya muda na sehemu, inayo jali upatikanaji wa washiriki na sehemu walipo”.

Washiriki walishukuru sana Atabatu Abbasiyya kwa kufanya semina hii muhimu, ambayo wamesoma mambo mengi muhimu na mageni kwa mujibu wa kauli yao, wakaonyesha kua ilikua fursa kubwa sana kwao wanatamani iendelee zaidi, wakakiombea kituo cha maarifa ya Qur’an na tafsiri yake na kuichapisha waendelee na mwenendo huu wa kuitumikia Qur’an na Ahlulbait (a.s), wakasema kua kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kwa semina za aina hii zinazo fundisha namna ya kufanya tafiti kuhusu Qur’an tukufu kwa kufuata mwenendo sahihi wa Qur’an na kizazi kitakasifu (a.s).

Kumbuka kua kituo hiki kimesha fanya semina nyingi za Qur’an na nadwa za kielimu kuhusu Qur’an na elimu zake pamoja na mwenendo wa vizito viwili, na wamefungua anuani maalumu kwa ajili ya kujibu na kutoa ufafanuzu kuhusu maswala ya Qur’an ambayo ni: m.t.t.q313@gmail.com kwa mawasiliano zaidi unaweza kupiga simu namba: 07602323733 au unaweza kuwapata katika mitandao ya kijamii (face book, whwatsapp, viber na telegram).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: