Ujumbe wa Ataba tukufu za Iraq katika hafla ya kuhitimisha ratiba ya wiki ya kitamaduni awamu ya nne (Nasimu Karbala) huko Pakistani..

Maoni katika picha
Rais wa ugeni wa Ataba tukufu Shekh Aadil Wakil alisisitiza kua, atakaye tafuta ukomo wa mwisho wa wafuasi wa Ahlulbaiti (a.s) hataweza, imedhihiri wazi katika kongamano hili kubwa, tumekusanyika kufanya kongamano la Nasimu Karbala Hussein (a.s) katika aridhi ya mbali –Pakistani-.

Aliyasema haya kwenye hotuba aliyo toa katika hafla ya kuhitimisha wiki ya kitamaduni awamu ya nne (Nasimu Karbala) iliyo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu kwa kushirikiana na chuo cha Alkauthar cha Pakistani na kushiriki Atabatu Alawiyya, Askariyya na Abbasiyya.

Aliongeza kusema kua: “Nakufikishieni salamu kutoka kwa viongozi wakuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya na Atabatu Abbasiyya tukufu, Shekh Abdulmahdi Karbalai na Sayyid Ahmad Swafi (d.i), wanakuombeeni dua ya taufiq na ushindi, kama ambavyo hatuwasahau daima ndugu zetu wapenzi waliopo ndani ya nyoyo zetu, wanao endelea kupigana tangu miaka mitatu iliyo pita hadi sasa, wanapambana na magaidi walio vamia aridhi tukufu ya Iraq na kuangamiza watu na mazingira, wamefanya unyama usio elezeka, wasio kua na heshima wala mipaka wamevua ubinadamu wao na kuitupa dini yao”.

Akabainisha kua: “Na nyie hapa Pakistani hamjasalimika na unyama wao, bado hatuja sahau mashahidi wa Arubainiyya walio uawa katika shambulio la kigaidi lililo tokea katika mji mtukufu wa Swiwaan ndani ya mkoa wa Sandi, na wakafanya shambulio lingine katika kitongoji cha Baarajnaar mkoa wa Khabir-bakhtuun yaliyo pelekea kuuawa kwa makumi ya watu wasio na hatia, mashambulio ya kigaidi kama hayo ndiyo wanakumbana nayo ngugu zenu wa Iraq kwa miaka kadaa sasa.

Akasisitiza kua: “Batili itaisha na haki itasimama na yanayo fanyika Mwenyezi Mungu anayaona, lazima itafika siku ambayo matatizo yataisha na wingu jeusi litaondoka katika nchi zetu Iraq na Pakistani na itatawala amani na usalama”.

Akaendelea kusema kua: “Tunaishi katika saa za mwisho za kongamano hili tukufu katika aridhi nzuri, tunasema: inatuhuzunisha kuwaacha, kutokana na tabia nzuri tuliyo ona kwenu, tunatoa shukravi za dhati kwa kila aliyechangia kufanikisha kwa wiki hii ya kitamaduni, tunamuomba Mwenyezi Mungu awawafiqishe watu wote na atukutanishe tena mwakani inshallah.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: