Atabatu Abbasiyya tukufu yafungua dirisha jipya la Qur’an kwa wanafunzi wa vyuo vya Iraq..

Maoni katika picha
Miradi mingi ya Qur’an inafanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo inalenga watu wa tabaka tofauti katika jamii pamoja na kujenga uwezo na vipawa vya Qur’an, mradi huu wa sasa unalenga walimu na wanafunzi wa vyuo, na unasimamiwa na ofisi ya harakati kuhusu Qur’an chini ya idara ya mahusiano na vyuo, ya Atabatu Abbasiyya tukufu. Unaingia moja kwa moja katika mradi wa kijana wa Alkafeel mzalendo, katika mahafali za Qur’an zinazo fanywa na wanafunzi wa vyuo mara moja kila wiki, kutokana na ratiba itakavyo pangwa, huandaliwa mahafali za Qur’an kwa kushirikiana na viongozi wa chuo pamoja na idara za Qur’an katika chuo husika, msomaji wa Qur’an Ustadh Amru Alaa kiongozi wa idara ya harakati kuhusu Qur’an aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Ofisi ya harakati kuhusu Qur’an imebeba majukumu mengi yanayo husu Qur’an, kuanzia kwa walimu wa Qur’an katika vyuo vikuu vya Iraq kwa kuwaandalia semina na warsha mbalimbali, pamoja na program zingine nyingi, na mambo yanayo husu wanafunzi kwa kuweka ratiba zinazo wavutia katika kitabu cha Mwenyezi Mugu mtukufu na kuwafanya waishi kwa kufuata mwenendo wa Qur’an tukufu, na miongini mwa ratiba hizo ni (kufanya mahafali za Qur’an katika vitengo vyao vya ndani ya chuo) ratiba inayo lenga kutumia muda wao wa mapumziko vizuri kwa kusoma na kutafakari kwa mazingatio kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Akaongeza kua: Halfa hizo hua na mambo mengi kama vile:

“Kwanza: Kusomwa Qur’an tukufu na wasomi wa kimataifa kutoka katika Atabatu Husseiniyya na Atabatu Abbasiyya.

Pili: Hutolewa mawaidha elekezi kwa wanafunzi kutoka kwa shekhe miongoni mwa mashekh wa kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya kutokana na mada iliyo pangwa.

Tatu: Kipindi cha maswali na majadiliano baina ya wanafunzi na mtoa mada, ambapo atajibu maswali na kutoa maelezo zaidi pale panapo hitaji ufafanuzi,

Nne: Hufanywa mashindano kwa kutolewa maswali na wanafunzi kuyajibu kisha wale watakao jibu vizuri hupewa zawadi”.

Alaa akabainisha kua: “Hakika mradi huu ni endelevu hadi tufikie vyuo vingi zaidi vya Iraq, na una athari nzuri kwa wanafunzi na umekubalika vizuri kwa walimu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: