Idara ya kunufaika na zana za Ataba yaendelea na maandalizi ya msafara wa Saaqi kwa ajili ya ibada ya Umra..

Maoni katika picha
Idara ya kunufaika na zana katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaindelea na ratiba ya msafara wa Saaqi iliyo anza miaka ya nyuma kwa ajili ya safari za Umra na kuzuru kaburi la Mtume Muhammad (s.a.w.w) na maimamu (a.s) walio zikwa Baqii pamoja na maeneo mengine matukufu ndani ya mji wa Maka na Madina, inatoa wito kwa wanaotaka kwenda Umra katika mwezi wa Shabani wafanye haraka kujisajili, ukizingatia kuna idadi maalumu inayo hitajika, safari itaanza baada ya ziara ya Shabaniyya (15 Shabani) kwa siku kidogo inshallah.

Kiongozi wa idara hiyo Sayyid Mustwafa Dhiyaau-dini aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Idara ya kunufaika na zana za Ataba inaendelea na maandalizi ya safari ya (Saaqi) kwa ajili ya kwenda katika nyumba ya Mwenyezi Mungu kufanya ibada ya Umra kwa wananchi wanaopenda kufanya hivyo kwa bei ya ofa, jambo kubwa zaidi kwetu ni kutoa huduma bora zaidi kwa watu watakao kwenda Umra, tumejiandaa kumpokea kila anaye taka kufanya Umra kutoka katika kila mkoa wa Iraq na kumpa huduma bora zaidi na kwa gharama nafuu”.

Akabainisha kua: Ratiba ni pamoja na:

  • 1-
  • 2- Kukaa siku nne katika mji wa Madina na siku sita katika mji wa Maka tukufu.
  • 3- Kutembelea maeneo matukufu ya Madina na Maka.
  • 4- Usafiri wa Madina na Maka tukufu (kutoka uwanja wa ndege wa Jida hadi Madina na Madina hadi Maka na kurudi uwanja wa ndege).

Siku ya kwanza: Kukutana katika kituo (karakana) ya Saaqi iliyopo barabara ya Maitham Tammaari kisha kuelekea uwanja wa ndege na kuanza safari ya Jida, kisha tutaelekea katika mji wa Madina Munawara halafu itafuata ratiba ya kugawa vyumba katika moja ya hoteli za mji huo,

Siku ya pili: Kutembelea msikiti wa Mtume mtukufu, kama muda utaruhusu tutatembelea na maimamu wa Baqii (a.s).

Siku ya tatu: Kutembelea maeneo matukufu ya mji wa Madina Munawara (Mashahidi wa Uhudi – Masjidi Qiblataini – Masaajid Sab’aa – Masjid Kuba).

Siku ya nne: Haina ratiba (mapumziko).

Siku ya tano: Kutakua na muda wa mapumziko, baada ya Adhuhuri wataondoka kuelekea katika Miqaat kwa ajili ya Ihraam, na baada ya magharibi wataondoka na kuelekea Maka na baada ya kufika watapewa vyumba vya kulala.

Siku ya sita: Kutekeleza ibada ya Umra.

Siku ya saba: Haina ratiba (mapumziko).

Siku ya nane: Kutembelea maeneo matukufu ya Maka (Jabal Thuur – Muzdalifa – Mina – Jabal Noor na makaburi ya Hajun).

Siku ya tisa: Kufanya Umra kwa niaba kwa watakao taka kufanya hivyo.

Siku ya kumi: Kurejea katika Nchi yetu kipenzi na kufika salama inshallah.

Gharama za kushiriki ni:

  • 1- Mtu mwenye umri wa miaka 12 na zaidi ni ($875) keshi, na kwa mkopo ni ($950).
  • 2- Mtoto kuanzia miaka 2 hadi 11 ni ($450) keshi, na kwa mkopo ni ($550).
  • 3- Malipo ya chumba cha peke yako kwa anaye taka ni ($200).

Pamoja na kuzingatia yafuatayo:

  • 1- Msafara utafatana na kiongozi wa idara pamoja na muelekezaji wa kidini.
  • 2- Kila siku watapata milo mitatu kwa ratiba ya wazi kwa wote.
  • 3- Unatakiwa kuleta paspoti yenye muda wa kuendelea kutumika zaidi ya miezi sita pamoja na kopi ya rangi ya kitambulisho cha uraia na picha tatu na paspot size.
  • 4- Anaye taka kusafiri kwa mkopo lazima adhaminiwe na mtumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na deni litalipwa kwa kukatwa katika mshahara wake, na anatakiwa kulipa ($200) na itakayo bakia itakatwa ($100) kila mwezi kwenye mshahara.
  • 5- Mkopo wa mtoto kuanzia miaka 2 hadi 11 atatakiwa kutanguliza ($100) na itakayo baki itakatwa ($50) kila mwezi katika mshahara wake.

Kwa maelezo zaidi na kushika nafasi, tembelea ofisi ya idara ya kunufaika na zana za Ataba iliyopo katika eneo la Babu Bagdad/ Jengo la imamu Hassan Askariy (a.s) zamani likiitwa (Funduq Dalla) au piga simu zifuatazo: (07801952463/ 07602283026).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: