Utukufu na a’amaali (Ibada) katika siku nyeupe za mwezi wa Rajabu..

Maoni katika picha
Hakika siku nyeupe katika mwezi wa Rajabu zina utukufu maalumu mbele ya Mwenyezi Mungu, Allah huongeza rehema zake kwa walimwengu ndani ya siku hizo, hivyo muislamu hatakiwi kupoteza fursa hii, hakika thawabu ambazo Mwenyezi Mungu huwapa waja wake wanaotenda wema katika siku hizo hakuna anaye weza kuzielezea.

Ameandika Sayyid ibun Twausi katika kitabu cha (Iqbaal) kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) anasema: (Atakaye funga siku tatu katika mwezi wa Rajabu na akasimama usiku wake katika siku ya mwezi kumi na tatu, kumi na nne na kumi na tano, naapa kwa yule aliye nituma kwa haki, hataondaka duniani ispokua kwa kukubaliwa toba yake, na kila siku aliyo funga atasamehewa madhambi makubwa sabini, na atakidhiwa haja sabini wakati wa kukata roho, na haja sabini wakati anapo ingizwa kaburini, na haja sabini atakapo toka kaburini, na haja sabini wakani wa mizani, na haja sabini wakati wa kupita katika siraatwa, ataandikiwa thawabu kana kwamba kila siku aliyo funga aliwaacha huru wafungwa sabini, na kana kwamba alihitimu Qur’an mara elfu sabini, na kana kwamba alitoka katika njia ya Mwenyezi Mungu miaka sabini, na kana kwamba alijenga katika njia ya Mwenyezi Mungu nyumba sabini, na atawaombea shufaa ndugu zake sabini walio hukumiwa moto, atajengewa katika pepo ya Firdausi miji elfu sabini, katika kila mji kuna qasri sabini elfu, katika kila qasri kuna mahuraini elfu moja, kila huraini ana watumishi elfu moja).

Kuhusu a’amaali (ibada) za siku hizi, imepokewa kutoka kwa imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s) anasema: (Umma huu umepewa miezi mitatu haijawahi kupewa umma mwingine wowote, Rajabu, Shabani na Ramadhani, na siku tatu hawajawahi kupewa wowote, usiku wa mwezi kumi na tatu, kumi na nne na kumi na tano katika kila mwezi, na umepewa sura tatu hazijawahi kupewa yeyote, Yaasin, Tabaaraka – Mulk na Qul huwa Llahu ahad, atakaye kusanya haya mambo matatu atakua amekusanya mambo bora yaliyo pewa umma huu). Akaulizwa: namna gani atakusanya hayo mambo matatu? Akajibu (a.s): aswali katika kila siku nyeupe miongoni mwa mwezi hiyo mitatu, usiku wa mwezi kumi na tatu rakaa mbili, katika kila rakaa asome surat Fat-ha na hizo sura tatu, na katika usiku wa mwezi kumi na nne aswali rakaa nne, katika kila rakaa asome surat Fat-ha na hizo sura tatu, na katika usiku wa mwezi kumi na tano aswali rakaa sita, katika kila rakaa asome surat Fat-ha na hizo sura tatu, atakua amepata utukufu wa miezi hii mitatu na atasamehewa dhambi zote isipokua ya shirki).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: