Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chawakumbuka majemedari wake waliopata shahada katika vita ya kukomboa mji wa Bashir..

Maoni katika picha
Sehemu ya katikati ya haramu mbili tukufu alasiri ya Juma Tatu (12 Rajabu 1438 h) sawa na (10 April 2017 m) pamefanyika hafla iliyo simamiwa na viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji ya kuwakumbuka majemedari watukufu walio jitolea kupambana na magaidi hadi wakapata shahada katika vita ya kukomboa mji wa Bashir kutoka mikononi mwa magaidi ya Daesh.

Hafla ilihudhuriwa na idadi kubwa ya viongozi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) pamoja na familia za mashahidi na idadi kubwa ya waumini, ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa, ukafuatiwa na ujumbe wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na Shekh Kamali Shahid miongoni mwa aliyo sema ni:

“Salam nyingi na amani na pongezi nyingi ziwaengee mashahidi ambao kutokana na wao Iraq imehifadhika na heshima na amani vimepatikana, Mwenyezi Mungu amekufanyeni kua sababu ya kutabasamu kwa watoto na kuhifadhika kwa maeneo matukufu, hakika nyie enyi mashahidi mmetukuka na mmekirimiwa kwa kunyanyua bendera ya uislamu, wallahi mlisema kauli ya haki kwa sauti ya juu: uwe mbali kwetu udhalili (Haihaata minnaa dhillah), mmejifunza kwa Hussein shahid na watoto wake pamoja na maswahaba zake namna ya kulinda heshima na kuondoa udhia, mmeshusha bendera ya batili na kuiweka chini ya nyayo, tunajifakhari kutokana na nyie enyi majemedari hakika nyie ndio utukufu wetu, mmepanda mmea na umetoa mauwa ya ubinadamu na haki imedhihiri, nyie ni watukufu zaidi mmeitikia wito wa Marjaa dini mkuu, na mkawa miongoni mwa watu bora kabisa mwa walio itikia, hongereni sana hakika mmefuzu kufuzu kuliko kukubwa”.

Kisha ukafuata ujumbe wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji ulio wasilishwa na kiongozi wake mkuu Ustadh Maitham Zaidiy alisema kua: “Tunafanya hafla hii kwa mnasaba wa kumaliza mwaka mmoja tangu kupata shahada kwa majemedari bora wa kikosi cha Abbasi (a.s) walio uawa katika aridhi ya Bashir kipenzi, wakaloanisha aridhi hiyo kwa damu zao tukufu kwa ajili ya kuikomboa kutoka mikononi mwa magenge ya kigaidi yaliyo kua yameidhibiti kwa zaidi ya mwaka, ndugu zangu watukufu kikosi cha Abbasi (a.s) kilikwenda Bashir kutokana na wito wa Marjaa dini mkuu na maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa wakili wake ambaye ni kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i), baada ya wakazi wa mji huo kuomba kwenda kuokolewa, kutokana na dhulma kubwa waliyo kua wakifanyiwa na magaidi, ndipo Hashdi Sha’abi tukaitikia wito wao, kikosi cha Abbasi (a.s) kikaingia vitani na kupigana kishujaa na kwa ujasiri mkubwa sana, kwa kujitolea kwao na damu zao takasifu tukafanikiwa kukomboa mji huo kutoka mikononi mwa magaidi na kuurudisha mikononi mwa wakazi wake ukiwa salama”.

Kisha ulifua ujumbe wa wakazi wa mji wa Bashir na ndugu wa mashahidi walio sifu namna wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) walivyo pambana kishujaa hadi wakafanikiwa kuukomboa mji huo kwa damu zao tukufu.

Halafu ikaonyeshwa filamu ya vita ya kukomboa mji wa Bashir kutoka mikononi mwa Daesh, kisha mshairi Abuu Hasanain Rabi’iy akaimba qaswida ya kimashairi iliyo elezea ushujaa walio onyesha wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) katika vita ya kukomboa mji wa Bashir, hafla ilihitimishwa kwa kupewa zawadi familia za mashahidi watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: