Tarehe kumi na tatu Rajabu Aswabu Kaaba yapata utukufu kwa kuzaliwa ndani yake Qur’an yenye kutamka bwana wa mawasii Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s)..

Maoni katika picha
Alimzaa ndani ya haram ya Mola wake, ndani ya ukumbi wa nyumba ya msikiti wake.

Nyeupe zimetakasika nguo zake, zimetukuka na umetukuka uzawa wake.

Katika siku kama ya leo –tarehe kumi na tatu Rajabu baada ya mwaka wa tembo kwa miaka thelathini- dunia inasherehekea kuzaliwa kwa Qur’an yenye kutamka, bwana wa mawasii, Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s) aliye zaliwa ndani ya Kaaba tukufu, hakuwahi kuzaliwa kabla yake wala hatozaliwa baada yake yeyote ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu zaidi yake, hiyo ni takrima na utukufu wa Mwenyezi Mungu kwake, na kutukuza hadhi yake.

Mama yake anaitwa bibi Fatuma bint Asad bun Hashim bun Abdulmanafi, na mke wake ni bibi Fatuma bint wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) aliishi miaka 63 na muda wa uimamu wake ulikua miaka 30 lakini muda wa serikali yake ilikua miaka 3.

Alilelewa imamu wetu Amirulmu-uminina (a.s) na Mtume (s.a.w.w) baada ya mtume kumchukua kwa Ammi yake Abuutwalib kwa ajili ya kumpunguzia ugumu wa maisha, hapa utafahamu kua imamu (a.s) alipata malezi bora ya kitabia na kibinadamu, aliyo fundishwa na Mtume (s.a.w.w), aliwahi sema imamu Ali (a.s) aliyo fundishwa na mtume wa Mwenyezi Mungu katika moja ya maneno yake: ((Hakika mnafahamu nafasi yangu kwa mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) ukaribu tulionao na nafasi yangu kwake, alinilea miguuni kwake na kunikumbatia kifuani nikiwa mtoto, na kunilaza kitandani kwake mwili wake ukigusana na mwili wangu, alikua anatafuna chakula kisha ananilisha, haijawahi kutokea ulimi wake ukasema uongo, wala kukosea katika vitendo, Mwenyezi Mungu mtukufu alimfungamanisha na malaika wa kumuongoza katika haki na tabia njema usiku na mchana, na mimi nilikua namfuta kama mtoto (wa mbuzi) anavyo mfuata mama yake, kila siku alinisomesha tabia njema na kuniamrisha nizifuate, kila mwaka nilikua pamoja naye katika pango la Hira ninamuona na hakuna yeyote mwingine aliye kua anamuona zaidi yangu)).

Miongoni mwa laqabu zake (majina ya sifa) (a.s) ni: Amirulmu-uminina, Imamul-muttaqina, Sayyidul-auswiyaa, Sayyidul-muslimina, Sayyidul-arab, Haidari (simba), Yaasubu-dini, Al-anzaulbatwin, Qaaidul-ghuri Muhajirin, Asadu-llahi wa Asadu Rasul… na mashuhuri zaidi ni laqabu ya Amirulmu-uminina.

Majina yake ya kunia (baba fulani) (a.s) ni: (Abuu Hassan, Abuu Hussein, Abuu Sibtwain, Abuu Rihanatain, Abuu Turabi) na kunia ya kwanza ndio mashuhuri zaidi.

Kuhusu kuzaliwa kwake (a.s) imamu Swadiq (a.s) anasema: ((Abbasi bun Abdulmutwalib na Yazidi bun Qa’anab walikua wamekaa baina ya genge la bani Hashim na bani Uzza karibu na nyumba ya Mwenyezi Mungu mtukufu, akaja bibi Fatuma bint Asadi bun Hashim mama wa Amirulmu-uminina (a.s), akiwa na ujauzito wa Amirulmu-uminina (a.s) wa miezi tisa, siku za kujifungua zilikua zimetimia.

Akasema: Akasimama kuelekea nyumba ya Mwenyezi Mungu, akiwa na dalili za uchungu, akaelekeza mikono yake mbinguni na akasema: Ee Mola! Mimi nakuamini, na ninaamini yaliyo kuja kutoka kwako kupitia mitume, na kila nabii miongoni mwa manabii wako, na kila kitabu ulicho teremsha, mimi ninasadikisha maneno ya babu yangu Ibrahim kibenzi chako, hakika mdiye aliye jenga nyumba yako hii tukufu, ninakuomba kwa haki ya nyumba hii na aliye ijenga, na huyu mtoto aliye tumboni mwangu anaye nizungumzisha na kuniliwaza kwa maneno yake, na mimi ninayakini kua ni moja ya alama zako na dalili zako nakuomba unifanyie wepesi uzazi wangu.

Abbasi bun Abdulmutwalib na Yazid bun Qa’anab wanasema: pindi alipoongea Fatuma bint Asadi na kuomba dua hiyo, tuliona Kaaba inafunguka na bibi Fatuma akaingia ndani na kutoweka machoni mwetu, halafu ikajifunga kama ilivyo kua, tukakimbilia ufunguo ili waingie baadhi ya kina mama wakamsaidie, mlango haukufunguka, tukajua hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu, akakaa humo siku tatu, ilipo fika siku ya tatu Kaaba ikajifungua palepale ilipo funguka mara ya kwanza, bibi Fatuma akatoka akiwa amemshika Ali (a.s) mikononi mwake, kisha akasema: Enyi watu, hakika Mwenyezi Mungu mtukufu ameniteua mimi miongoni mwa waja wake, na kanitukuza katika wateule wake walio tangulia, alimteua Asia bint Muzahim, hakika alimuabudu Mwenyezi Mungu kwa siri sehemu ambayo watu walio muabudu walipata madhara (waliteswa), na akamteua Maryam bint Imran na akamfanyia wepesi katika kumzaa Issa, akatikisa mtende na ukamdondoshea tende zilizo iva vizuri. Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu ameniteua mimi na amenifanya kua bora zaidi yao, na zaidi ya wanawake wote walio tangulia kabla yangu, kwa sababu mimi nimejifungua ndani ya nyumba yake tukufu, na nimekaa humo siku tatu nakula matunda ya peponi, nilipo taka kutoka huku nimemshika mwanangu nimesikia sauti ikiniambia: Ewe Fatuma mwite mwanao “Ali” hakika mimi ni Aliyul-Aala, na mimi nimemuumba kutokana na uwezo wangu, utukufu wangu, uadilifu wangu na nimetoa jina lake katika jina langu, nitamuadabisha adabu ninazo ridhia na nitampa amri zangu, na nitampatia elimu yangu, amezaliwa katika nyumba yangu, atavunja masanamu na kuyatupa, atanitukuza na kuniabudu, atakua imamu baada ya kipenzi changu na mtume wangu mmbora wa viumbe wangu Muhammad, na atakua wasii wake, wamefaulu watakao mpenda na kumnusuru, ole wao watakao muasi na kumpuuza na kumnyang’anya haki yake)).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: