Ugeni wa Ataba tukufu wafanya marekebisho ya mwisho katika ratiba ya kongamano la Amirulmu-uminina (a.s) la kitamaduni awamu ya tano na wasisitiza kua litakua la aina yake..

Husseiniyya litakapo fanyika kongamano
Ugeni wa Ataba tukufu (Alawiyya, Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya) unao shiriki katika kongamano la Amirulmu-uminina (a.s) la kitamaduni awamu ya tano litakalo fanyika katika Husseiniyya ya Fadhlu Nisaai katika mji wa Kalkata nchini India kuanzia (14 - 19 Rajabu 1438 h), chini ya kauli mbiu: (Amirulmu-uminina (a.s) ni hoja kwa waja na muongoaji katika wema) kwa usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wamesisitiza kua kongamano hili litakua la aina yake na litaendeleza mazuri ya makongamano manne yaliyo pita, yanayo endana na hadhi na utukufu wa Ataba kiroho na kitamaduni.

Hayo yalizungumzwa katika kikao cha maandalizi kilicho fanywa na ugeni huo ndani ya eneo litakapo fanyika kongamano hilo na kufanya marekebisho ya mwisho katika ratiba.

Ustadh Jasaam Saidiy mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano na maonyesho katika Atabatu Abbasiyya tukufu ameuambia mtandao wa Alkafeel kilicho jiri katika kikao hicho kua: “Kikao kimejadili mambo mengi, miongoni mwa yaliyo jadiliwa ni:

Moja: Kuainisha waongeaji miongoni mwa wawakilishi wa Ataba na shakhsiyya za kihindi.

Mbili: Kujadili mambo yatakayo fanyika katika siku za kongamano na kuongeza yale yanayo faa kuongezwa kutokana na umuhimu wake.

Tatu: Kujadili wageni maalum (shakhsiyya) walio alikwa katika kongamano hili.

Nne: Kuandaa jaduali maalumu linalo anyesha ziara zitakazo fanywa na ugeni wa Ataba za kuwatembelea watu (shakhsiyya) binafsi na taasisi za kidini katika mji wa Kalkata.

Tano: Kuipa nafasi kubwa ratiba ya visomo vya Qur’an tukufu katika kongamano hili, ambayo watashiriki wasomaji wa Ataba tukufu kwa sababu inaathari zaidi.

Sita: Tumejadili kuhusu kutembelea makumbusho ya mji huu na sehemu za nakala kale (makhtutwaat) kwa ajili ya kufungua ushirikiano nao katika sekta hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: