Kamati ya maandalizi ya kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu yaonyesha vikao vyake na maandalizi ya kongamano hilo..

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu, asubuhi ya siku ya Juma Tano (14 Rajabu 1438 h) sawa na (12 April 2017 m), ilikutana katika Atabatu Abbasiyya tukufu katika vikao vyao vya kila wiki vya maandalizi ya kongamano hilo litakalo fanyika mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Shabani.

Kamati hiyo baada ya kuhudhuria wajumbe wake wote walijadili mambo mengi, yakiwemo yanayo husu mialiko na vyeti vya ushiriki pamoja na kuhimiza kamati washirika kukamilisha maandalizi ya kongamano hili la kumi na tatu.

Rais wa kamati ya maandalizi Sayyid Afdhal Shaami alisema kua: “Kikao cha leo kilikua cha kuonyesha mambo yaliyo kamilika katika kipindi hiki miongoni mwa maandalizi ya kongamano, kuna kamati zimekamilisha majukumu yao na zipo ambazo bado na zimehimizwa zikamilishe”.

Akabainisha kua: “Tumekubaliana kuanzia wiki ijayo tufanye vikao mara tatu kwa wiki, na baada ya wiki hiyo tutakutana kila siku hadi siku ya ufunguzi wa kongamano”.

Wajumbe wa kamati ya maandalizi na rais wa kamati ya matangazo Sayyid Aqil Yasiriy wamesema kua: “Kutokana na kukaribia kwa kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu, kamati ya maandalizi imesha kamilisha mambo mengi, na leo tumekubaliana baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na namna ya uendeshaji wa hafla, na kushiriki kwa baadhi ya watu kupitia email wakiwa katika balozi zao au nchi zao, na tumebadilisha walio toa udhuru wa kuto shiriki na kuweka wengine”.

Sayyid Muyassir Hakim mkuu wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa Karbala alisema kua: “Leo tumejadili mambo mengi yanayo husu mialiko binafsi, pamoja na kuainisha watu watakao itwa kutoka ndani ya Iraq, na tumeandaa utaratibu maalumu wa mialiko ambao utafatwa na kamati ya uhusiano na mialiko, pamoja na hayo tumeandaa vitambulisho na vyeti vya ushiriki vitakavyo gawiwa kwa washiriki wa kongamano na washiriki wa maonyesho ya vitabu”.

Hakim akaongeza kusema kua: “Tumekamilisha makubaliano na baadhi ya vyuo vikuu vya Iraq kutuandalia wakalimani wa lugha tano tofauti kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano kwa baadhi ya wageni wapatao (100), na kuandaa jopo la watumishi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) watakao simamia mapokezi ya wageni”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: