Kutolewa zawadi kwa washairi walio shiriki: Kumalizika kongamano la imamu Ali (a.s) la watunzi wa mashairi..

Maoni katika picha
Imefanyika hafla ya kuhitimisha kongamano la imamu Ali (a.s) katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu alasiri ya Ijumaa (16 Rajabu 1438 h) sawa na (14 April 2017 m), lililo endeshwa na ofisi ya washairi kwa kusaidiana na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Ali kwa watunzi wa qaswida), lililo dumu siku mbili kwa vikao vinne, kila siku vikao viwili vya mashairi, kwa ushiriki wa makumi ya washairi kutoka katika mikoa tofauti ya Iraq, kongamano hili ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bwana wa ufaswaha Amirulmu-uminina (a.s).

Hafla ya ufungaji wa kongamano hilo iliyo hudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) na jopo la viongozi wa Ataba tukufu, ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ikaanza majlisi ya mashairi murua, washairi walipanda kwenye mimbari mmoja mmoja na kusoma qaswida na mashairi ya kumsifu Amirulmu-uminina (a.s) na kuonyesha mapenzi kwake.

Kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) aliongea machache katika hafla hii, miongoni mwa aliyosema ni: “Tunawakaribisha sana sehemu hii tukufu, na tunafuraha kubwa kwa kuja kwenu kutoka mikoa tofauti kushiriki pamoja nasi katika siku hizi za kukumbuka kuzaliwa kwa Amirulmu-uminina (a.s), hakika mashairi ni ujumbe, na husaidia kukomaza fikra na kujenga maelewano, mashairi yamehifadhi uarabu wetu na lugha yetu, namshukuru Mwenyezi Mungu aliye wawezesha waandaaji wa kongamano hili, hakika tunaburudika kwa mashairi, na hauza kwa ujumla inategemea sana mashairi, hutoleo ushahidi wa mashairi katika mambo mengi, kuna aina nyingi za mashairi yanayo fungamana na masomo rasmi, kwa sababu shairi limekaa vizuri kimuundo na kimatamshi, na hueleweka zaidi katika baadhi ya maeneo, Shekh Mudhafar (q.n) na baadhi ya wanazuoni wameweka fani ya ushairi katika masomo ya msingi matano, yajulikanayo kama (swana’atu khamsa) ambayo ni: (swana’atu burhaan, swana’atul jadal, swana’atul mughaalatwa, swana’atul khitwaaba na swana’atu shi’iri)”.

Hafla ilihitimishwa kwa kutolewa zawadi kwa washairi wote walioshiriki katika kongamano hili, tunategemea kuendelea kwa makongamano kama haya, kwa sababu yanaboresha mafungamano ya jamii na lugha yao ya kiarabu asilia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: