Chuo cha masomo ya kibinadamu chaingia mkataba wa kujenga jengo jipya na chasisitiza kua hiyo ni hatua ya kwanza ya kukifanya kua chuo kikuu kamili..

Maoni katika picha
Chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa baraka za kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmad Swafi (d.t), chuo cha masomo ya kibinadamu kilicho chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeingia mkataba na shirika la Liwaau Al-alamiyya wa kujenga jengo kamili lenye sifa za kimataifa linano endana na maendeleo ya kiwango cha elimu ya kimataifa.

Mkataba umesainiwa baina ya chuo cha masomo ya kibinadamu kilicho wakilishwa na dokta Swafaa Abduljabaar Ali Mussawiy na shirika la Liwaau Al-alamiyya lililo wakilishwa na Sayyid Aadil Maalik Abdurahmaan kiongozi mtendaji wa shirika hilo, pande mbili hizo zimekubaliana kujenga majengo mapya ya chuo yenye sifa za kimataifa pamoja na jengo la dispensary, maktaba na kumbi za mikutano ikiwemo na sehemu za watumishi, bustani na viwanja vya michezo.

Mkuu wa chuo amesisitiza kua ujenzi huu ni msingi wa kuelekea katika kukifanya kua chuo kikuu kamili, wamekubaliana kuendelea na utekelezaji wa hatua ya pili ya (ujenzi wa vyumba vya madarasa ya chuo cha masomo ya kibinadamu), awamu ya kwanza itakua katika kiwanja namba (94496/3) chenye ukubwa wa (Dunam 32 na Aulak 4 na 3.75m) kilichopo katika mji wa Najafu Ashrafu/ kisiwani.

Kumbuka kua kwa sasa chuo kipo katika mji wa Najafu Ashrafu/ Kufa tukufu karibu na malalo ya swahaba mtukufu Maitham Tamaar (r.a), majengo yake hayaendani na maendeleo ya sasa pia hayaendani na ongezeko la wanafunzi, hivyo ilikua ni muhimu kutafuta sehemu kubwa inayo endana na malengo yake. Chuo kilianza na kitengo cha (sheria na katiba) kikiwa na wanafunzi (104) hadi mwaka wa masomo 2015 – 2016 chuo kilikua na wanafunzi (5098) na wahitimu walifika (1570) na sasa hivi kina vitengo sita: (sheria na katika, uhandisi na sayansi ya kompyuta, udaktari wa meno, mbinu za uchambuzi, uuguzi na habari) na kinawanafunzi (2455) wavulana na wasichana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: