Hospitali ya Alkafeel yawapa miguu bandia wapiganaji watano wa Hashdi Sha’abi na kuwazidishia matumaini..

Maoni katika picha
Toka kutolewa kwa fatwa tukufu ya kuilinda Iraq na maeneo yake matukufu hospitali ya rufaa Alkafeel sawa na taasisi zingine za Atabatu Abbasiyya tukufu, imechukua jukumu la kuwasaidia majeruhi wa Hashdi Sha’abi na kuchangia katika kupunguza maumivu yao kadri ya uwezo wake, kutokana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu yanayo himiza kufanya hivyo, hospitali ya Alkafeel imefanya mambo mengi sana kwa wapiganaji wa Hashdi Sha’abi nafasi haitoshi kuyataja hapa, miongoni mwake ni hili lililo fanywa hivi karibuni la kutoa miguu sita ya bandia kwa wapiganaji watano walio poteza miguu yao katika vita ya kukomboa aridhi ya Iraq kutoka mikononi mwa magaidi ya Daesh.

Kiongozi mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel dokta Haidari Bahadeli amebainisha kua: “Hospitali ya Alkafeel inafanya kila iwezalo kwa wapiganaji wa Hashdi Sha’abi na wanajeshi wa serikali, tunatoa msaada wowote unao hitajika na kwa uwezo wetu wote, hivi karibuni; kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) tumeagiza miguu bandia ya wapiganaji watano wa Hashdi Sha’abi kutoka Swiden, katika mashirika mawili ya nchi hiyo yenye uwezo mkubwa wa kutengeneza viungo bandia, na kazi ya kuwafunga miguu hiyo imefanywa kwa ushirikiano kati ya wataalamu wa Swiden na wa Iraq”.

Akaongeza kusema kua: “Vifaa walivyo fungwa vipo vya aina mbili: kuna vifaa tambuzi na vya kawaida, vina uwezo wa kumsaidia mtu kutembea kawaida, na kuwarudishia jambo walilokua wamepoteza, hivyo kuwapa matumaini mapya, jambo hili ni muhimu sana kwa sasa kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia”.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali, tembelea toghuti yetu ifuatayo: (www.kh.iq) au kiga simu namba: (07602344444 au 07602329999).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: