Maktaba na Daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya maonyesho ya urepeaji wa nakala kale na utunzaji wake katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya..

Maoni katika picha
Miongoni mwa maonyesho ambayo hufanyika ndani na nje ya mkoa wa Karbala, ni yale yanayo fanywa na kituo cha kurepea na kutunza nakala kale cha maktaba na Daru makhtutwaat chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambacho sasa hivi kinafanya maonyesho ya urepeaji wa nakala kale pamoja na kutambulisha kazi zake, maonyesho haya yanafanyika katika chuo cha Mustanswiriyya ndani ya ukumbi wa maktaba kuu ya chuo hicho, maonyesho haya ni sehemu ya kuimarisha kushirikiana na kusaidiana baina yao.

Shekh Mahmood Swafi wa idara ya kurepea nakala kale na utunzaji wake alisema kua: “Hakika maonyesho haya ni sehemu ya kuonyesha uwezo wa Atabatu Abbasiyya katika sekta hii ambao haupatikani katika taasisi zingine na kujenga ushirikiano baina ya Ataba na taasisi zingine katika sekta ya kurepea nakala kale na utunzaji wake”.

Naye rais wa chuo cha Mustanswiriyya dakta Swadiq Hamaash alisema kua: “Hakika hii ni fursa nzuri sana, kupitia maonyesho haya tunaona uwezo iliyo nao Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya utunzaji wa nakala kale, kupitia maonyesho haya tumefahamu juhudi kubwa inayo fanywa na kituo hiki kwa ajili ya kuhifadhi turathi hizi, Inshallah maonyesho haya itakua ni chachu ya kufanyika maonyesho mengine na kujenga ushirikiano baina yetu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: