Maukib ya maombolezo ya imamu Kadhim (a.s) yaanza kutembea kutoka uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Nyoyo zenye huzuni na majonzi makubwa kutokana na tukio la kufariki kishahidi imamu wa saba wa Ahlulbait (a.s) imamu Mussa bun Jafari (a.s), kutokana na utaratibu wa maombolezo ulio andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuhuisha mnasaba huu, baada ya Adhuhuri ya leo ratiba ya maombolezo ilianza katika malalo ya babu yake imamu na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maukib (kundi) la waombolezaji lilianzia katika uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), watumishi wa Ataba hiyo waliokua wakiomboleza msiba huu walijipanga mistari na wakaanza kuimba qaswida za huzuni na wakaondoka kuelekea katika malalo ya Sayyid Shuhadaa na babu wa imamu Abuu Abdillahi Hussein (a.s) wakiwa wamebeba jeneza la kuigiza la imamu madhlumu aliye uawa kwa sumu Mussa Kadhim (a.s), wakatembea hadi katika Atabatu Husseiniyya tukufu walipo pokelewa na watumishi wa Ataba hiyo kwa qaswida za maombolezo zilizo jenga hisia za huzuni kubwa kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), msiba ulio tokea katika siku kama ya leo mwezi ishirini na tano Rajabu mwaka 183 h.

Katika maombolezo haya walishiriki makatibu wakuu wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) na idadi kubwa ya viongozi na wakuu wa vitengo vya Ataba hizo pamoja na kundi kubwa la mazuwaru watukufu.

Kumbuka kua Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya ) hufanya ratiba maalumu za maombolezo katika tarehe za kufariki kwa Ahlulbait (a.s) katika kipindi chote cha mwaka, na matembezi yao imma huanzia katika Atabatu Abbasiyya hadi katika Atabatu Husseiniyya au kunyume chake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: