Kisomo cha mashairi: Ilikua ndio hitimisho la ratiba ya siku ya pili ya kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni awamu ya kumi na tatu..

Kisomo cha mashairi
Kwa mashairi murua yaliyo iga ufasaha wa imamu Hussein (a.s) ilikamilishwa ratiba ya siku ya pili ya kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu (4 Shabani 1438 h) sawa na (1 May 2017 m) kwa mujibu wa ratiba ya kongamano.

Kisomo cha mashairi murua yaliyo zikonga (zifurahisha) nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s), kilihudhuriwa na idadi kubwa ya wageni wa kongamano la Rabiu Shahada pamoja na viongozi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) na idadi kubwa ya mazuwaru watukufu, kilifanyika katika haram ya Abulfadhil Abbasi na kufunguliwa kwa Qur’an tukufu, baada ya Qur’an washairi mahiri walianza kusoma mashairi yao, kwanza kabisa alipanda mimbari mshairi Ahmad Murshidi kutoka Karbala, kisha akafuatia mshairi Ali Harzi kutoka Kuwait, baada yake akaingia Sefu Zabun kutoka Baabil, walisoma mashairi mazuri sana yaliyo aksi maneno ya imamu Hussein (a.s) na kuhuisha kumbukumbu ya watakatifu walio zaliwa katika mwezi wa Shabani.

Halafu ikafuata Qaswida ya mshairi Husaam Hamzawiy kutoka katika mji wa Hamza magharibi, kisha ikafuata Qaswida ya mshairi Maitham Faalih kutoka Bagdad, kisha Haidar Gharibawiy kutoka Waasit, akafuata Haidar Shiyaai kutoka Karbala na msomaji wa mwisho alikua ni Muhammad A’ajibiy kutoka Muthana katika vitongoji vya Samaawah, ambaye beti za mashairi yake zilielezea kwa ufasaha watukufu walio zaliwa katika mwezi wa Shabani na kuonyesha upendo mkubwa kwa imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), hafla ilihitimishwa kwa kugawa zawadi na vyeti vya ushiriki kwa washairi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: