Washairi waeneza ladha ya beti zao katika malalo ya imamu Hussein (a.s)..

Kisomo cha mashairi
Jopo la washairi limeendesha kisomo cha qaswida na mashairi katika ukumbi wa Sayyid Auswiyaau (a.s) katika Atabatu Husseiniyya tukufu, kisomo hicho ni miongoni mwa ratiba za kongamano la Rabiu Shahada awamu ya kumi na tatu, linalo endelea sasa hivi chini ya usimamizi wa Atababa mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) kisomo hicho cha mashairi kimehudhuriwa na wageni wa kongamano pamoja na mazuwaru.

Kikao hicho kilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu washairi mahiri wa kiiraq na kutoka katika nchi zingine za kiarabu wakaanza kusoma mashairi yao, yaliyo konga (furahisha) nyoyo za wasikilizaji kwa sauti nzuri na ujumbe murua ulio onyesha mapenzi ya dhati kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) ambapo tunaishi katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa nuru za Shaabaniyya.

Katika kisomo hiki walishiriki washairi wafuatao: (Muhyi Dini Jaabiriy kutoka Najafu, Aqeel Liwaatiy kutoka Oman, Misaar Riyadh kutoka Basra, dokta Ali Zalikhan kutoka Sirya, Swalaah Silaawi kutoka Karbala, Muan Ghalib kutoka Qadisiyya, Ahmad Khayyal kutoka Baabil, Abdu Zuhrah Ausiy kutoka Karbala), mashairi hayo yalikua na vituo vifupi vya Qaswida za kumsifu mtume zilizo somwa na Mula Yaasin Waailiy.

Washairi walitoa shukrani za dhati kwa kamati ya maandalizi kwa kuwapa fursa ya kusimama mahala hapa patakatifu na kusoma beti zao zenye ujumbe mzuri, wamesema huo ni utukufu mkubwa na heshima ya pekee waliyo pewa, hayo waliyasema katika mahojiano mbalimbali yaliyo fanywa baada ya kumaliza ratiba hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: