Ataba mbili tukufu zafunga kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu..

Maoni katika picha
Baada ya siku tano zilizo jaa ratiba za mambo ya kielimu na kitamaduni, vikao vya utafiti, Qur’an, mashairi na ziara, pamao na mikutano mbalimbali, alasiri ya Alkhamisi (7 Shabani 1438 h) sawa na (4 May 2017m) katika ukumbi wa imamu Hassan (a,s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanyika hafla ya kuhitimisha kongamano la Rabiu Shahada awamu ya kumi na tatu, lililo fanywa kwa kusimamiwa na kugharamiwa na Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) chini ya kauli mbiu: (Imamu Hussein (a.s) ni kisima kirefu na chemchem endelevu).

Hafla hiyo ilipata mahudhurio makubwa ya wanazuoni wa kidini na kisekula wa ndani na nje ya Iraq pamoja na wawakilishi wa mazaru tukufu, hali kadhalika wawakilishi wa serikali ya Karbala na viongozi wakuu wa kisheria wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) na makatibu wakuu wao pamoja na ndugu wa mashahidi wa Hashdi Sha’abi.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukafuata ujumbe wa Ataba mbili tukufu ulio wasilishwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Husseiniyya tukufu muheshimiwa Shekh Abdulmahad Karbalai (d.i), alisema kua: “Hakika vita ya kitamaduni inayo enda sambamba na vita ya kutumia siraha hivi sasa dhidi ya makundi ya takfiri na kigaidi, inahitaji kubainisha kwa watu kuhusu mwenendo potovu wa makundi ya takfiri na magaidi ambao leo hii wanatumia mitandao kutangaza poropaganda zao, mitandao inanguvu kubwa ya kuharibu akili za vijana na kutumbukia katika fikra na mwenendo mbaya wa makossa ya jinai…”.

Baada yake ulifuata ujumbe wa wageni wa kiiraq walio shiriki katika kongamano hili na uliwasilishwa na Shekh Sarmad Tamimiy muwakilishi wa Daru Iftaai ya Iraq, ambye alisema kua: “Enyi ndugu! katika siku hizi tunasherehekea kuzaliwa kwa miezi ya Hashimiyya (a.s), minara ya uongofu na taa ziangazazo katika kongamano lililo pewa jina la: (Kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu) kongamano ambalo umekusanyika ugeni huu mtukufu kutoka dini tofauti madhehebu na nchi tofauti, wamekusanyika kutokana na mapenzi na kufuata usia alio tuachia bwana mtume (s.a.w.w) alipo sema: (..Nakuachieni vitu ambavyo mkishikamana navyo hamta potea, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha watu wa nyumbani kwangu).

Na wageni kutoka nchi za nje walikua na ujumbe vilevile ulio wasilishwa na muwakilishi wa nchi za ulaya wa zamani katika mashariki ya kati na mkuu wa kutafuta maelewano ya kimataifa Elias Karook, ambaye alisema kua: “Katika siku nilizo kaa hapa nimeona kwa imamu Hussein (a.s) kuna alama ya uadilifu hakika nimeathirika sana na yote niliyo shuhudia hapa na nikirudi ulaya nitaenda kusimulia..”.

Baada yake alipanda mshairi Najaah Arsani, akawaburudisha kwa Qaswida ya kishairi iliyo athiri sana wasikilizaji, Qaswida ilimuhusu bibi zainabu (a.s) namna alivyo vumilia maudhi aliyo fanyiwa baada ya kuawa kaka yake imamu Hussein (a.s) katika atdhi ya Karbala.

Halafu akafuatia dokta Jamali Dabaagh katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya tukufu, ambaye alizungumza kwa niaba ya Ataba tukufu za Iraq, akasema kua: “Haifichiki kwa wageni watukufu kua Ataba za Iraq zina kazi nyingi na moja ya kazi zake ni kueneza elimu ya kitamaduni, makongamano haya hufanyika kila mwaka, harakati za Ataba hazija jifunga katika makongamano tu, kuna mikutano mingi na machapisho ya kielimu mbalimbali pamoja na vituo vya utafiti, yote haya kwa ajili ya kuhudumia watu na kuwaongoza katika dini yao tukufu, alhamdulilahi yamefanikiwa yaliyo fanikiwa na tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwafikishe zaidi.

Pia kulikua na usomaji wa Qur’an tukufu, iliyo somwa na msomi wa kiiran Haafidh wa Qur’an Muhammad Ali Islamiy, baada yake ikawekwa filamu ya: (Sayyidul Maai) iliyo tengenezwa na ofisi ya picha za video chini ya idara ya enternet katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Baada ya hapo viongozi wakuu wa kisheria wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) wakasimama pamoja na makatibu wao wakuu na wakaanza kutoa zawadi kwa baadhi ya familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi, wakahitimisha kwa kuwapa zawadi baadhi ya wageni wa kongamano na vyombo mbalimbali vya habari vilivyo changia katika kurusha matukio ya kongamano ya moja kwa moja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: