Kwa kuthamini juhudi zao: Uongozi mkuu wa Atba mbili tukufu watoa zawadi kwa wana habari walio tangaza matukio ya kongamano la Rabiu Shahada..

Maoni katika picha
Baada ya Aduhuri ya Ijumaa (8 Shabani 1438h) sawa na (5 May 2017m) katika ukumbi wa Sayyid Auswaiyaai (a.s) ndani ya Atabatu Husseiniyya tukufu ilifanyika hafla ya kutoa zawadi kwa vyombo vya habari (Luninga, Redio, Magazeti na mitandao ya Intanet) walio tangaza matukio ya kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu lililo dumu siku tano kuanzia 3 – 7 Shabani.

Hafla hii imefanyika pembezoni ya kongamano la Rabiu Shahada kama sehetu ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kuonyesha kuthamini kwao juhudi zilizo fanywa na wanahabari katika kutangaza matukio ya kongamano.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu, halafu Sayyid Aqeel Yasiriy mjumbe wa kamati ya maandalizi akaongea, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakuna asiye fahamu juhudi zilizo fanywa na vyombo vya habari kuanzia siku ya kwanza ya ufunguzi wa maonyesho ya vitabu hadi siku ya mwisho katika hafla ya kuhitimisha, wamekua wakitangaza matukio yote ya asubuhi na jioni, kuna yaliyo rushwa moja kwa moja na mengine yalirekodiwa”.

Akabainisha kua: “Kuna chanel nyingi za luninga (tv) ambazo sio rahisi kuzipata lakini kamati ya habari iliweza kupata chanel zaidi ya (30), ukiongeza na magazeti na idhaa za Ataba mbili tukufu, watangazaji wa kiarabu na wa kigeni wote walifurahia mambo yanayo fanywa na Ataba hizi tukufu, wamejionea wenyewe mwenendo na maendeleo ya Ataba, pamoja na mazingira magumu ambayo taifa linapitia kwa sasa, vita kali inayo endendelea na njama za kudhofisha nchi za ndani na nje, pia pamoja na mazingira magumu bado Ataba zimefanya kongamano hili ambalo lilianzishwa kuonyesha kua wairaq ni wamoja kwa baraka za imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Katika kumalizia maneno yake akasema kua: “Tunaomba samahani kwa upungufu wowote ulio jitokeza, inawezekana mtu alijisahau akakosea hili au lile (udhuru kwa watu wakarimu hukubaliwa). Naomba samahani kwaniaba ya watumishi wote na mimi mwenyewe, hizi zawadi tunazo wapa ni ndogo sana bila shaka maimamu watukufu tulio wakumbuka ndio watakao kuzawadieni”.

Baada ya hapo ikagawiwa midani, zawadi na vyeti vya ushiriki kwa wanahabari na mawakala wa luninga magazeti redio na mitandao ya intanet walio tangaza matukio ya kongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: