Zaidi ya aina mia mbili: Atabatu Abbasiyya tukufu yashiriki maonyesho ya vitabu ya kimataifa Tehran awamu ya thalathini..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa Tehran awamu ya thalathini, yanayo fanyika chini ya kauli mbiu: (Ili tusome kitabu kingine) katika majengo ya maonyesho huko Shamsi “Shahri Aaftab” kusini ya mji mkuu Tehran.

Atabatu Abbasiyya tukufu imewakilishwa na kitengo cha habari na utamaduni walio jaza katika kabati (shelfu) zao zaidi ya aina mia mbili za vitabu vyenye maudhui tofauti, zikiwemo za fiqhi, dini, malezi, sekula na majarida mbalimbali yenye lugha nyepesi inayo faa kwa watu wa tabaka zote, hili ndilo huleta mvuto mkubwa kwa watu wanaokuja kutembelea maonyesho.

Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki kwa mara ya nane katika maonyesho haya, na imeyaweka katika orodha ya maonyesho ya kimataifa inayo takiwa kushiriki, maonyesho haya ni sawa na maonyesho yaliyo pita, machapisho waliyo nayo Ataba yametolewa na Ataba kuanzia uandishi uhakiki na uchapaji na hayapatikani sehemu nyingine, hii ndio tofauti kubwa iliyo nayo Ataba ukilinganisha na vituo vingine.

Tawi la upambaji limepata sifa kubwa kutoka kwa kiongozi wa idara ya intanet Sayyid Haidari Twalib Abdul-amiri, wamejenga banda lao katika umbo la haram tukufu, juu yake kuna kubba inayo fanana na kubba ya dhahabu na nguzo zinazo shikilia kubba zinafanana na minara miwili, hali kadhalika shelfu zake zinafanana na sehemu za jenge zilizopo katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na katikati yake wameandika jina la tawi.

Kumbuka kua maonyesho haya yamehusisha vituo vya usambazaji wa vitabu (2700) vya kitaifa na kimataifa, miongoni mwake vituo (110) kutoka katika nchi za kiarabu, ushiriki wetu ni fursa ya kuangalia na kujuana na vituo vingine vya usambazaji, aidha ni fursa pia ya kuitangaza Atabatu Abbasiyya tukufu na huduma inazo toa pamoja na maendeleo inayo pata katika sekta ya elimu, utamaduni na ujenzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: