Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la Bagdad yafanya hafla ya Qur’an kwa mnasaba wa kufunga mwaka..

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la Bagdad iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya mahafali kubwa ya Qur’an kwa mnasaba wa kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya mitukufu katika siku za mwezi huu wa Shabani, mahafali hii imefanyika kama sehemu ya kusherehekea kufikisha mwaka wa tatu tangu kuanzishwa kwa tawi hili la Maahadi, pamoja na kupongeza ushindi wanaopata wapiganaji wetu katika viwanja vya vita.

Katika mahafali haya wameshiriki wasomi wakubwa wa Qur’an kama vile: (Sayyid Hussein Halo, na msomi wa kimisri Said Saiid, na Ali Jawaad, na Hafidh Hussein, aliye shika nafasi ya tatu katika mashindano ya Qur’an ya kimataifa ya thalathini na nne huko Iran), mahafali hii ilipata mahudhurio makubwa kutoka kwa wadau wa Qur’an, wanajamii na majemedari wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) pamoja na kundi kubwa la waumini.

Ustadh Nabil Saadiy mkuu wa Maahadi ya Qur’an tawi la Bagdad alielezea maendeleo waliyo pata katika kipindi cha miaka mitatu iliyo pita, ikiwa ni pamoja na kuendesha hafla za Qur’an, mashindano na semina za Qur’an tukufu, akatoa shukrani nyingi kwa kila aliye changia mafanikio hayo, yaliyo fikiwa kwa baraka ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na ikhlasi ya watumishi wake, akamuomba Mawenyezi Mungu awawafikishe zaidi katika kuvitumikia vizito viwili vitukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: