Usiku wa nusu ya mwezi wa Shabani uzawa mtukufu

Maoni katika picha
Imamu Mahadi (a.f) ni miongoni mwa maimamu wa Ahlulbait (a.s) naye ni imamu wa mwisho katika maimamu kumi na mbili alio wabashiri Mtume (s.a.w.w) alipo sema: Baada yangu watakuja maimamu kumi na mbili wote wanatokana na makuraish, nao ni katika kizazi kitakasifu cha bibi Fatuma na miongoni mwa wajukuu wa imamu Hussein (a.s).

Uzawa matukufu

Ilikua ni kawaida ya bibi Hakima (bint wa imamu Jawaad a.s) na shangazi wa imamu Hassan Askariy (a.s), kila anapo mtembelea anamuomba Mwenyezi Mungu amruzuku mtoto wa kiume, anasema: Siku moja niliingia kwake (kwa imam Hassan a.s) nikaomba kama ambavyo hua naomba, akasema: ewe shangazi yangu hakika mtoto ambaye umekua ukimuomba Mwenyezi Mungu aniruzuku anazaliwa usiku wa leo, ewe shangazi yangu leo lala hapa kwetu, hakika usiku wa leo atazaliwa mtoto mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu, kupitia huyo Mwenyezi Mungu ataihuisha aridhi baada ya kufa, bibi Hakima akasema: kutoka kwa nani? Simuoni bibi Narjisi akiwa na ujauzito, akasema: kutoka kwa bibi Narjisi hakuna mwingine.

Akasema: Nikamfuata bibi Narjisi nikamgeuza na kumuangalia mgongoni na tumboni sikuona athari ya mimba, nikarudi nikamuambia nilivyo fanya, akatabasamu kisha akaniambia: Itakapo fika Alfajiri utaiona hiyo mimba, hakika huyu mfano wake ni kama alivyo kua mama yake Nabii Mussa (a.s) mimba yake haikuonekana, hakuna yeyote aliye jua hadi wakati wa kujifungua, kwa sababu Firaun alikua anapasua matumbo ya kina mama wajawazito kwa ajili ya kumtafuta Mussa na huyu ni mfano wa Mussa (a.s).

Bibi Hakima akasema: Nilimchunga usiku wote hadi Alfajri huku akiwa amelala mbele yangu hakugeuka kulia wala kushoto, ilipo fika alfajiri ujauzito ukadhihiri, nikamkumbatia (bibi Narjisi) kifuani kwangu, imamu Askariy (a.s) akasema: msomee (Innaa anzalnaahu fii lailatil qadri) nikaanza kumsomea, nikamuuliza vipi hali yako? Akasema: limetokea jambo alilo kuambia maulana, nikaendelea kumsomea kama nilivyo amrishwa, mtoto akanipokea kutoka tumboni kwa mama yake akawa anasoma kama nilivyo kua nasoma na akanitolea salamu.

Bibi hakima akasema: nikashtuka kwa nilicho sikia, imamu Askariy (a.s) akaniambia: usishangae hekima ya Mwenyezi Mungu mtukufu anamtamkisha kwa hekima ndogo na atamfanya kua hoja kubwa katika aridhi, kabla hatuja kamilisha maneno bibi Narjisi akatoweka, kana kwamba kumewekwa pazia kati yetu, nikaenda kwa imamu Askariy (a.s) huku nikiita, imamu akaniambia: Rudi ewe shangazi yangu utamkuta palepale.

Akasema: Nikarudi baada ya muda mfupi nikamuona, kana kwamba pazia imeondolewa kati yetu akiwa na nuru, mara nikamuona mtoto (a.s) akiwa amesujudu huku ameinua mikono juu na anasema: (Nashuhudia ya kwamba hakuna mungu ispokua Allah mmoja asiye na mshirika na hakika babu yangu ni mtume wa Mwenyezi Mungu na baba yangu ni Amirulmu-uminina kisha akataja imamu mmoja baada ya mmoja hadi akafikia kwake mwenyewe.

Akasema (a.s): Ewe Mwenyezi Mungu timiza ahadi yangu, na ukamilishe jambo langu na ukithibitishe kisimamo changu na ujaze dunia amani na uadilifu kupitia mimi...)
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: