Mwisho wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa ya Tehran: Kiongozi wa maonyesho asisitiza kua ushiriki wa Atabatu Abbasiyya ulikua mzuri na wenye manufaa..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni wamemaliza maonyesho ya vitabu huko Tehran awamu ya thelathini ambayo yalidumu kwa siku kumi, zaidi ya taasisi na vituo vya usambazaji wa vitabu (2700) walishiriki, miongoni mwake (110) vituo vya kiarabu, maonyesho hayo yalifanyika kwenye eneo la maonyesho katika mji wa Shamsi (Shahru Aaftaab) chini ya kauli mbiu isemayo: (Ili tusome kitabu kingine).

Maonyesho haya –sawa na maonyesho nane yaliyo pita- yalikua na mafanikio makubwa, tulipata muitikio mkubwa, pamoja na idadi kubwa ya washiriki lakini tulivutia watu wengi hususan wadau wa tamaduni, elimu za sekula na dini, tulikua na zaidi ya aina (200) za vitabu vinavyo lenga watu wa tabaka zote, hivyo watu wote walivutiwa na sisi wairan na wasio kua wairan.

Mwisho wa maonyesho haya yalitangazwa matokeo ya washindi wa mashindano yaliyo endeshwa na Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) kuhusu historia ya imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ambapo jumla ya watu (15) wameibuka washindi na Ataba mbili tukufu zimewazawadia gharama ya ziara zao nchini Iraq, hafla hiyo ilihudhuriwa na waheshimiwa na kidini, kitamaduni na kijamii pamoja na idadi kubwa ya washiriki na wadau wa maonyesho, ikiwa ni pamoja na mkuu wa maonyesho haya Abbasi Swalehiy, ambaye alisisitiza kua: “Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu bega kwa bega na taasisi za kitaifa na kimataifa katika maonyesho haya, kuna faida kubwa na ni fursa muhimu ya kufahamiana na kuwasiliana, na tunaomba waendelee kushiriki katika maonyesho yajayo..” aliwasifu pia watumishi wa Ataba kwa juhudi kubwa za kiutendaji walizo onyesha katika kipindi chote cha maonyesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: