Wanahitajika walimu wa masomo yote, ikiwa ni pamoja na elimu ya Nafsi na malezi, mtu atakaye tuma maombi atatakiwa kuandaa somo la mfano katika fani yake miongoni mwa masomo ya msingi, na atatakiwa kuwasilisha vielelezo vifuatavyo:
- 1- Vielelezo vinne.
- 2- Cheti cha kuhitimu masomo au waraka wowote unao thibitisha hilo.
- 3- Picha mbili za paspot size.
Maombi yawasilishwe katika idara ya shule ya Saaqi ya wavulana iliyopo katika mtaa wa Baladiyya nyuma ya Daru Dhiyaafah Karbala, ndani ya siku mbili (Juma Pili na Juma Tano) katika kila wiki, kuanzia (21/05/2017m) na katika mwezi wote wa Ramadhani.
Walimu watakao leta maombi watafanyiwa mahojiano baada ya mwezi wa Ramadhani pamoja na kupewa nafasi ya kusomesha somo la mfano kuanzia (02/07/2017m) kutokana na mawasiliano ya simu yatakayo fanyika.