Kuanza kwa kongamano la amani la kitamaduni awamu ya tisa katika mkoa wa Diwaniyyah..

Maoni katika picha
Jana Juma Nne (18 Shabani 1438h) sawa na (15 May 2017m) shughuli za kongamano la amani la kitamaduni awamu ya tisa zilianza, linalo simamiwa na uongozi wa Imamu Swadiq (a.s) wa kitamaduni kwa kushirikiana na Ataba za Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya na Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo: (Njia ya kukutana na kuonana katika jamii ndio moyo wa maelewano), katika kongamano hili wameshiriki watafiti na wasomi wa kihauza na kisekula kutoka ndani na nje ya Iraq, kongamano litadumu siku nne, ni sehemu ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa imamu Mahdi (a.f).

Kongamano hili limehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya na makatibu wakuu wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) na jopo la viongozi wa Ataba, pamoja na idadi kubwa ya wadau muhimu wa kidini, kitamaduni na kisekula, kongamano lilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukafuata ujumbe kutoka kwa kamati ya usimamizi wa kongamano ulio wasilishwa na Shekh Aqeel Ali Zubaidiy, miongoni mwa aliyo sema ni: “Wakati ambao wapiganaji wetu wanaendelea kupata ushindi dhidi ya magaidi na kuendelea kujinasua kutoka katika makucha yao na wasaidizi wao, zinafanyika juhudi za kuharibu fikra na maadili ya jamii kwa kutumia mwanya huu ambao watu wanashughulika na vita pamoja na kusaidia wapiganaji na wakimbizi kutokana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu.

Kutokana na ukweli huo tunakuta kua majukumu yamekua mengi na ya aina tofauti, miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu katika mji huu, hususan uongozi wa Imamu Swadiq (a.s) wa kitamaduni, wasimamizi wakuu wa kongamano hili, ni kupata nafasi ya kuchangia swala hili, na fahari kubwa kwetu ni kupata nafasi ya kumtumikia Baqiyyatu Llah (a.f), Alhamdu lilaahi tumeendelea kupata neema hii ya kufanya makongamano haya hadi sasa hivi ni mwaka wa tisa mfululizo, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu mtukufu na baraka za Marjaa dini mkuu na msaada wa Ataba tukufu, tunamuomba Mwenyezi Mungu aijalie nchi yetu amani na baraka”.

Kisha ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na kiongozi mkuu wa kisheria Sayiid Ahmad Swafi (d.i), miongoni mwa aliyo sema ni: (Waumini wanatakiwa kuwafahamu Ahlulbait (a.s) kwa usahihi na kwa undani, ili wasidumbukie katika mtego wa mashetani wa kibinadamu wanao potosha imani sahihi ya uislamu, huku wakidai kua wanahusiana na imamu Mahdi (a.f), kuna baadhi ya watu wamekua na ujasiri wa kudai kua wanampenda imamu na wapo karibu nae zaidi jambo ambalo sio sahihi, watu hao wangepuuzwa na kutopata watu wa kuwasikiliza wasinge endelea na madai yao hayo batili…”.

Halafu ukafuata ujumbe wa wageni washiriki ulio wasilishwa na Shekh Abdulhamid Nashmiy kutoka Ihsaa, alianza kwa kupongeza kufanywa kwa kongamano hili kutokana na mnasaba wa kuzaliwa kwa imamu Muntadhar (a.f).

Akabainisha kua: “Hakika kongamano hili linafikia malengo ya wasubiriaji ya kimataifa na linalea kizazi baada ya kizazi, linachangia katika kujenga jamii inayo mtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake pamoja na imamu wa zama (a.f) alhamdu lilahi kwa baraka za kongamano hili na juhudi zinazo fanyika tumefikia ushindi na imebaki kidogo sana kupata ushindi kamili, tunamuomba Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi wetu na awatie nguvu wapiganaji na walinzi wa nchi hii kipenzi ambao ni jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi”.

Pia kulikua na ujumbe kutoka kwa kiongozi wa waandishi wa habari wakiiraq wanao ishi jijini Washinton (Marekani) ulio wasilishwa na Ustadhi Nizaar Haidari ambaye alisema kua: “Tunatakiwa kua miongoni mwa wanusuru wa Imamu (a.f) tuwe tayari wakati wote, hii inamaanisha tunatakiwa kushinda kila mtihani unao tusibu, mtihani mkubwa tunao kumbana nao ni kutenda mema na kua na imani thabiti, muumini mwenye matendo mema anapo kutana na mitihani Mwenyezi Mungu humsaidia kuishinda, msaada wa Mwenyezi Mungu hupatikana kwa waja wema, jambo muhimu tunalo takiwa kuishi nalo ni kudumisha uadilifu”.

Kongamano lilipambwa na mashairi pamoja na Qaswida mbalimbali za kumsifu imamu Mahdi (a.f) pia kulikua na Qaswida ya kuisifu Iraq na raia wake, mwishoni mwa kongamano hilo washiriki walielekea katika uzinduzi wa maonyesho ya vitabu na picha yaliyo fanywa na matawi ya Ataba mbalimbali tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: