Muendelezo wa harakati zake kuhusu Qur’an tukufu: Maahadi ya Qur’an (tawi la India) yafanya hafla ya Qur’an tukufu..

Maoni katika picha
Muendelezo wa hafla za Qur’an zinazo fanywa na Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya, tawi la Maahadi lililopo katika mji wa Qadhaa huko India wamefanya hafla ya Qur’an katika Husseiniyya ya mwezi wa bani Hashim iliyopo katika mji huo, hafla hii iliyo pata mahudhurio makubwa ni sehemu ya kueneza misingi ya Qur’an katika jamii.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha vikafuata visomo vya Qur’an vya wasomi mahiri ambao ni: (Muhammad Abudiy, Ali Murtadha Ifaariy, Hafidh Muhammad Mudhafar, Mula Zuhair Barqaawiy), kisha ukafuata ujumbe wa Sayyid Haamid Mar’abiy kiongozi wa tawi la Maahadi katika nchi ya India, akazungumzia hafla za Qur’an wanazo fanyaga na umuhimu wa kufuata mafundisho ya Qur’an na kuchukua mazingatio kutoka kwa Ahlulbait (a.s), halafu akaelezea baadhi ya harakati mpya zinazo fanywa na Maahadi.

Katika hafla hii yalifanyika mashindano yaliyo husisha vipengele tofauti vya Qur’an, mwishoni mwa hafla zikagawiwa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la India hufanya hafla nyingi za Qur’an kwa lengo la kusambaza mafundisho ya Qur’an tukufu, pia hufanya visomo vya Qur’an na huendesha semina za kuhifadhi Qur’an pamoja na kufundisha hukumu za usomaji wake na mengineyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: