Atabatu Abbasiyya tukufu yatoa tamko la kukanusha kumiliki chanel yeyote ya luninga (tv)..

Maoni katika picha
Katika tamko lake: Atabatu Abbasiyya tukufu imekanusha kumiliki chanel yeyote ya luninga (tv) yenye jina la Abulfadhil Abbasi (a.s) au moja ya majina ya sifa zake.

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetoa tamko hilo, na mtandao wa Alkafeel umefanikiwa kupata nakala yake, ambalo ni jibu la swali lililo ulizwa na jopo la waandishi wa habari, kama Atabatu Abbasiyya inamiliki kituo cha luninga (tv) kwa jina lake, au laa?

Tunakuletea nakala ya tamko na picha yake, pamoja na swali lenyewe:

Kwa: Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Tunahitaji ufafanuzi

…Asalam alaikum

Sio jambo geni kwenu kushirikiana na waandishi wa habari kutoka katika vituo mbalimbali, miongoni mwake vituo vya luninga (tv), katika kazi zetu za kila siku tunaona na kufanya kazi na vituo vingi vikiwemo ambavyo vimebeba jina la Abulfadhil Abbasi (a.s), baadhi yetu wanadhani kua ni kituo cha Atabatu Abbasiyya tukufu, je! Ni kituo chenu? Je! Atabatu Abbasiyya inamiliki kituo chochote cha luninga?

Tunatarajia kupata ufafanuzi kutoka kwenu kwa kujibu swali hili, kutokana na umuhimu wa vyombo vya habari na yale yanayo rushwa na vituo hivyo, hasa mambo yanayo husu Atabatu Abbasiyya tukufu, Mwenyezi Mungu atakulipeni heri…

Jopo la wanahabari.

Tamko

…Asalam alaikum wa rahmatu llahi wa barakatuhu

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya unasisitiza kua, haumiliki kituo chochote cha luninga (tv), wala hauna uhusiano na kituo chochote cha tv chenye jina la Abulfadhil Abbasi (a.s) au moja ya majina ya sifa zake…

Muhandisi Muhammad Abdulhussein Ashiqar

Katibu mkuu
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: