Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu atembelea maonyesho ya taasisi ya Nurul Hassan (a.s) Alkairiyya na awasifu wasimamizi wake..

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i) ameisifu taasisi ya Nurul Hassan (a.s) Alkhairiyya, moja ya taasisi zinazo toa misaada katika mkoa wa Karbala, kutokana na juhudi yao ya kusaidia mayatima, wajane pamoja na familia za mafakiri, baada ya kutembelea maonyesho yanayo fanyika katika eneo la baina ya haram mbili tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Kusaidia wajane na mayatima kunang’arisha matendo mema).

Katika matembezi haya alifuatana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Sayyid Muhammad Ashqari (d.t) na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi, walipokewa na mkuu wa taasisi hiyo Sayyid Issa Husseiniy na aliongozana nao wakati wakitembea korido (meza) za maonyesho hayo, na kukagua vitu vilivyo tengenezwa na wajane, mayatima na familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi na familia za mafakiri, ambampo kuna vitu tofauti ikiwa ni pamoja na: (michoro, kuchimba katika mbao, kuchora katika vioo na hati za kiarabu za aina mbalimbali) pia kulikua na vifaa vya kazi za mikono (ushonaji, kudarizi, kutengeneza majoho ya wanawake, mikeka na vifaa vilivyo tengenezwa kwa majani ya mitende) pamoja na kitengo cha picha za mnato zinazo onyesha mambo yanayo fanywa na taasisi.

Baada ya kukamilisha matembezi yao kiongozi mkuu wa kisheria alionyesha kufurahishwa sana na vitu alivyo viona, vinavyo onyesha namna taasisi hii inavyo wajali na kuwasaidia pamoja na kulea vipaji vyao na kubaini uwezo wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: