Watu wa Hilla: Tunawaambia walimwengu toeni kila mlie naye na sisi tunakutoleeni alama ya Iraq na uislamu Sayyid Sistani (d.dh.w)..

Maoni katika picha
Sayyid Sistani amekua alama kuu ya taifa kwa raia wa tabaka zote, tunaye jivunia mbele ya walimwengu wote, na tunawaambia toeni kila mlie naye miongoni mwa watu watukufu kwenu na sisi tutakutoleeni alama ya Iraq na uislamu Aayatullah Sayyid Sistani (d.dh.w).. haya yalisemwa na watu wa Hilla katika ujumbe wao ulio wasilishwa na Muhandisi Hassan Hilliy mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano la mazazi ya imamu Hassan Almujtaba (a.s) lililo anza jioni ya Juma Mosi ya jana katika bustani za sehemu ya Radu Shamsi ndani ya mji wa Hilla.

Akaongeza kua: “Enyi ndugu watukufu; tulipo amua kurejesha kongamano za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mkarimu wa Ahlulbait (a.s) lililo fanywa kwa mara ya kwanza mwaka (1386h) sawa na (1960m) zaidi ya miaka hamsini na tano iliyo pita, utawala wa kipindi kile ukazuia haraka kuendelea kwa kongamano hilo mwaka wa (1961m sawa na 1387h), haikutujia katika akili zetu ispokua kutegemea kila jambo zuri kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, leo hii tunafanya kongamano la kumi, tumejiona kua tumekua mfano bora wa kauli isemayo: (kitakacho fanywa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hustawi), chini ya kauli mbiu: (Imamu Hassan Almujtaba –a.s- ni hekima ya amani na utukufu wa uislamu) kwa usimamizi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) tunafanya kongamano la kumi la kukumbuka kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w)”.

Akabainisha kua: “Hafla ya mwaka huu imesadifu furaha za ushindi wanao pata wapiganaji wetu wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi watukufu, walio ingia vitani kutokana na fatwa ya Muheshimiwa Sayyid Sistani (d.dh.w) ambaye amekua alama ya taifa kwa raia wote na tunajivunia kwa walimwengu wote na tunawaambia: toeni mlio nao katika watu watukufu kwenu na sisi tutakutoleeni alama ya Iraq na uislamu Aayatullah Sayyid Sistani Mwenyezi Mungu amuhifadhi fahari ya umma wa kiislamu na bendera ya kudumu inshallah, tunatoa salamu za heshima na utukufu kwa kila aliye changia katika kulinda aridhi, heshima na raia, wapiganaji wa Iraq walio ifundisha dunia ushujaa na ujasiri kwa hakika wanastahili sifa kubwa”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Enyi wahudhuriaji watukufu kwa ruhusa yenu natoa shukrani za dhati kwa mtumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) Muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i) ambaye anafuatilia maandalizi ya kongamano hili yeye mwenyewe, daima anarejea kauli yake mashuhuri: (Tuna mapungufu katika kutekeleza haki ya imamu wetu Hassan Almujtaba –a.s-) namuambia kua: unahaki ya kujifaharisha kwani mafanikio makubwa yamepatikana kutokana na utukufu wa Mweenyezi Mungu na baraka za imamu Almujtaba (a.s) pamoja na juhudi zako, shukrani za dhati zimuendee pia Muheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya tukufu ambaye ametufungulia milango yote ya ushirikiano toka mwanzo wa uongozi wake, na shukrani za pekee ziwafikie pia makatibu wakuu wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), na kila aliye changia kufanikiwa kwa kongamano hili tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: