Sauti za mashairi ya kumpenda imamu Hassan (a.s) zapamba kumbukumbu ya kuzaliwa kwake kutukufu..

Maoni katika picha
Siku ya pili ya kongamano la mkarimu wa Ahlulbait imamu Hassan Almujtaba (a.s) linalo fanywa na watu wa Hilla chini ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) likiwa na kauli mbiu isemayo (Imamu Hassan –a.s- ni hekima ya amani na utukufu wa uislamu) limeshuhudia kikao cha usomaji wa mashairi jioni ya jana Juma Pili (15 Ramadhani 1438h) sawa na (11 Juni 2017m) kwa kushiriki idadi kubwa ya washairi, tukio hili lilifanyika katika bustani ya sehemu ya Radu Shamsi katika mji wa Hilla mkoa wa Baabil.

Kikao kilifunguliwa kwa Qur’an tukufu na kusomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha yakafuata mashairi mengi yaliyo somwa kuhusu utukufu wa imamu Hassan (a.s), hali kadhalika kikosi cha uimbaji wa qaswida za kiislamu cha Atabatu Husseiniyya chini ya usimamizi wa Ustadh Ali Kaadhim waliimba Qaswida nyingi kuhusu imamu Hassan (a.s), vilevile mtumishi wa Ahlulbait (a.s) Twalibu Faraati alisoma Qawsida mbalimbali kuhusu Ahlulbait (a.s) na ushujaa wa Hashdi Sha’abi watukufu.

Kisha yakasomwa mashairi mbalimbali kuhusu mkarimu wa Ahlulbait imamu Hassan (a.s) ambapo washairi wafuatao walishiriki: (Muhammad Aajibiy kutoka Samawa, Zainul-abidina Saidiy kutoka Karbala, Hussam Hamzawiy na Muhammad Fatwimiy kutoka Baabil).

Kikao hicho kilihitimishwa kwa kutoa zawadi kwa wapiganaji wa imamu Hassan Almujtaba (a.s) na mtoto wa marehemu Kaadhim Mandhuur Karbalai.

Washairi walitoa shukrani nyingi kwa kamati ya maandalizi ya kongamano hili kutokana na kuendelea kufanya kongamano hili kila mwaka, ikiwa ni pamoja na kuwapa nafasi ya kushiriki na maendeleo mazuri yanayo patikana mwaka baada yam waka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: