Kufuatia semina zilizo pita myaka ya nyuma Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza kuanza uandikishaji wa wanafunzi watakao shiriki katika masomo ya Qur’am kipindi cha kiangazi yatakayo anza baada ya Iddi Fitri tukufu –Inshallah- katika mji wa Karbala na katika matawi yake yote yaliyopo kwenye mikoa mingine, uandikishaji utaendelea hadi (25 Juni 2017m).
Masomo ya kiangazi huendeshwa kutokana na kauli ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: (Waadabisheni watoto wenu mambo matatu: kumpenda Mtume wenu, kuwapenda watu wa nyumbani kwake na kusoma Qur’an), kutokana na maelekezo ya Atabatu Abbasiyya tukufu masomo hayo yatahusisha: (Kuhifadhi Qur’an tukufu, Fiqhi, Aqida na Akhlaq).
Kila anayependa kushiriki katika masomo haya anakaribishwa kujiandikisha katika ofisi ya makao makuu ya Maahadi iliyopo Karbala karibu na haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mkabala na mlango wa imamu Mussa Alkaadhim (a.s), kwa watakaopenda kujiandikisha katika makao makuu ya Maahadi, amma wale wa mikoani wanaweza kujiandikisha katika matawi moja kwa moja, kujiandikisha kunafanyika kwa kujaza fomu maalumu, na muombaji anatakiwa alete picha za paspoti saizi mbili na kopi ya kitambulisho cha uraia.
Kumbuka kua kutakua na wahadhiri mahiri katika Qur’an tukufu na mahaafidh pamoja na baadhi ya watumishi walio hitimu masomo katika Maahadi, zitafundishwa mada tofauti, zikiwemo za Fiqhi, Aqida na Akhlaq, na namna ya kuhifadhi Qur’an tukufu na kuisoma kwa usahihi, hali kadhalika zitafundishwa hukumu za swala, swaumu, udhu, kuoga na mengineyo.