Waumini wahuisha usiku wa tatu wa Lailatul Qadri ndani ya maeneo matakasifu ya malalo ya imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Usiku wa tarehe ishirini na tatu Ramadhani ni usiku wa tatu wa Lailatul Qadri, nao ni usiku bora zaidi kushinda siku mbili za nyuma, kuna hadithi nyingi zinazo sema kua siku hiyo ndio siku la Lailatul Qadri ambayo hukadiriwa kila kitu katika usiku huo, usiku huu una ibada maalumu tofauti na siku mbili za nyuma, kundi la waumini wamekuja kuhuisha usiku huu mtukufu kwa kufanya ibada ndani ya malalo matakasifu ya imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), hufunga safari katika usiku huu na siku mbili za nyuma kuja Karbala mji wa imamu Hussein (a.s), usiku wa Lailatul Qadri kutokana na umuhimu wake kiimani, kila mu-umini anakusudia kupata fadhila za usiku huo, waumini wanao huisha usiku huo kwa kufanya ibada huzagaa maeneo mbalimbali, wengine huingia ndani ya uwanja wa haramu tukufu za imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na wengine hufanya ibada katika uwanja wa katikati ya haram mbili na sehemu za karibu na haram.

Kundi la waumini wametekeleza ibada zao kwa kusoma Qur’an tukufu, kuswali na kusoma dua zilizo pokelewa na watu wa nyumba ya mtume (a.s), na waliomba kwa wingi dua ya kuharakisha faraja ya imamu wa zama, na Mwenyezi Mungu aihifadhi Iraq na watu wake na kila baya na awarehemu mashahidi wa jeshi la serikali na hashdi sha’abi na awaponye haraka majeruhi wao, awarejeshe salama wapiganaji katika familia zao wakiwa na ushindi, wameomba ushindi wa haraka na kukombolewa kwa eneo la aridhi lililobaki.

Watumishi wa vitengo vyote katika Ataba Mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) wamefanya kila wawezalo kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji wa ibada, wametandika mazulia eneo lote, wameweka maji baridi kila kona na wamejaza misahafu na vitabu vya dua na ziara kila sehemu, pia wameandaa magari ya kubeba watu hadi katika eneo la Ataba tukufu na wameyaweka katika barabara zoto zinazo ingia eneo la haram.

Usiku wa tarehe ishirini na tatu ni miongoni mwa siku za Lailatul Qadri ambao haulinganishwi na usiku wowote ule kwa utukufu, kufanya ibada ndani ya usiku huo ni sawa na kufanya ibada miezi elfu moja, katika usiku huo hukadiriwa riziki za waja na hushuka malaika kwa imamu Mahdi (a.f) na kumuonyesha makadirio hayo, huondoa alitakalo na hubakiza alitakalo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: