Hivi punde: Ofisi ya Muheshimiwa Ayatullah Sayyid Sistani (d.dh.w) yatangaza kua kesho Juma Tatu ni siku ya kwanza ya Iddul-Fitri tukufu..

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa dini mkuu Muheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Hussein Sistani (d.dh.w) imetangaza rasmi kua kesho Jumatatu (26 Juni 2017m) ni siku ya kwanza ya mwzi mtukufu wa Shawwal (1438h) na ni siku ya kwanza ya Iddul-Fitri.

Mtandao wa kimataifa Alkafeel na wataalamu wake wote kwa niaba ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) tunatoa mkono wa pongezi kwa umma wa kiislamu na Maraajii wetu watukufu pamoja na raia wa Iraq bila kuwasahau wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kwa sikukuu hii, tunamuomba Mwenyezi Mungu atukubalie ibada zetu na ibada zenu, na aijalie Iraq amani na utulivu, awanusuru wanajeshi wetu na majemedari wa Hashdi Sha’abi watukufu, awape ushindi katika vita vyao dhidi ya maadui wa dini na taifa, na awarehemu mashahidi wa Iraq na kuwaingiza peponi, na aponye majeruhi wao hakika yeye msikivu wa dua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: