Maahadi ya Qur’an tukufu –tawi la Landan- yakamilisha semina zake za Qur’an katika mji wa Bermingham Uingereza..

Maoni katika picha
Miongoni mwa vipaombele na harakati zinazo fanywa na tawi la Maahadi ya Qur’an tukufu tangu ilipo funguliwa katika mji mkuu wa Uingereza Landan, ni kuendesha semina za Qur’an katika ofisi zake au maeneo mengine ya nchi hiyo, imekua ikifanya hivyo toka kuanzishwa kwake kwa lengo la kuinua kiwango cha Qur’an kwa watu na jamii ya Uingereza hasa wahamiaji waarabu wanao ishi huko, zimeendeshwa semina mbalimbali za Qur’an kutokana na umuhimu wa kujifundisha kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu.

Hivi karibuni Maahadi imekamilisha semina kadhaa zilizo endeshwa katika mji wa Bermingham Uingereza zilizo husisha makumi ya washiriki wavulana na wasichana wenye umri tofauti, wamefundishwa usomaji sahihi wa Qur’an kwa kufuata hukumu za tajwid na adabu za usomaji pamoja na kuhifadhi juzu la thelathini “juzu Amma”.

Hafla ya kukamilisha semina hizo ilihudhuriwa na mkuu wa Maahadi Shekh Dhiyaau-Dini Zubaidiy, ambaye alisisitiza umuhimu wa kufanyika semina hizi, zinazo changia sana katika kueneza utamaduni wa Qur’an kwa wana jamii, akawashukuru wasimamizi wa semina hizi kutokana na juhudi kubwa wanayo fanya ya kufundisha Qur’an kwa kutumia mbinu za kisasa zinazo endana na umri wa washiriki.

Washiriki walitunukiwa vyeti kutoka Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya, aidha walimu walio simamia semina hizi wakapewa zawadi kutokana na juhudi zao za kuandaa kizazi kinacho fuata maadili ya Qur’an na mwenendo wa Ahlulbait (a.s).

Washiriki wa semina hizi walisifu kazi nzuri inayo fanywa na Maahadi ya Qur’an ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuendesha semina hizi zinazo saidia sana kuinua kiwango chao cha elimu ya Qur’an tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: