Miongoni mwa juhudi zake tukifu katika kuhakikisha inafundisha maadili mema kwa mayatima na kuchangia katika kuandaa jamii bora, na kuondoa hali ya unyonge ambayo huwakumba mayatima, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha watoto na makuzi wameweka hema la utoaji wa mafunzo ya kimaadili kwa ajili ya kunufaika na kipindi cha likizo za majira ya joto (kiangazi), wakiweka ratiba ya kuongeza kiwango cha elimu kitamaduni, ki-itikadi, uchumi na afya kwa mayatima na kuwawezesha kuishi vizuri, ili kuwatengenezea mazingira bora yatakayo wawezesha kuishi vizuri na familia zao pamoja na jamii kwa ujumla.
Ratiba hii inatekelezwa kwa mujibu wa hadithi za bwana Mtume na maelekezo ya maimamu wa Ahlulbait (a.s), yanayo sisitiza na kuhimiza kuwajali watu hawa na kuwapa usaidizi wa aina zote, hakika Atabatu Abbasiyy tukufu imebeba jukumu la kuwalea na kuwatunza mayatika na kuwapa mafunzo mbalimbali kutokana na wajibu wake kisheria na kimaadili, miongoni mwa program zake ni hema hili ambalo huwekwa kila mwaka kwa ajili ya mayatima.
Program hii inaendeshwa katika jengo la Shekh Kuleiniy (q.s) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ikihusisha mambo mbalimbali; ikiwa ni pamoja na kutolewa mihadhara ya kidini inayo endana na umri wao pamoja na kiwango cha elimu zao, safari za mapumziko katika maeneo ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) ikiwa ni pamoja na kuyatembelea malalo ya imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi (a.s), bila kusahau ratiba ya michezo mbalimbali, ratiba zote zinasimamiwa na mashekhe watukufu pamoja na maustadhi wenye uwezo mkubwa katika sekta hizo.