Kupongezana kufuatia ushindi mkubwa wa wairaq kwa kukombolewa mji wa Mosul: Chuo cha masomo ya kibinadamu chafanya hafla ya kuzizawadia familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abiy..

Maoni katika picha
Chuo cha masomo ya kibinadamu chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na taasisi ya Birru Rahim ya misaada ya maendeleo, wameandaa hafla ya kuzizawadia familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abiy sambamba na kusherehekea ushindi wa raia wa Iraq ulio patikana hivi karibuni kutokana na juhudi kubwa za jeshi la Iraq na Hashdi Sha’abiy kwa kukomboa mkoa wa Mosul kutoka mikononi mwa magaidi ya Daesh.

Hafla ilifanyika katika ukumbi mkubwa wa chuo na ilikua na mahudhurio makubwa ya wawakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na idadi kubwa ya walimu na wakuu wa vitengo pamoja na wanafunzi wa chuo, aidha kulikua na kundi kubwa la wanafamilia za mashahidi watukufu.

Mkuu wa chuo, Pr. Swafaa Abduljabaar Ali Mussawiy alisema kua: “Hakika ushindi uliopatikana wa kukomboa mji wa Mosul, unatokana na Mwenyezi Mungu mtukufu, hakika ni ushindi kwa Marjaiyya, ukiongozwa na Marjaa dini mkuu Sayyid Ali Sistani (d.dh), aliye toa fatwa takatifu iliyo tenganisha vita ya wema na vita ya shari, na baina ya haki na batili, na dhulma na uadilifu, fatwa hii ni muendelezo wa msimamo wa babu yake imamu Hussein (a.s) mbele ya dhulma na ukafiri”.

Akaongeza kusema kua: “Tunapo wazawadia wanafamilia wa mashahidi wetu, ni wazi kua wao ndio watu bora na wanastahiki kila aina ya heshima na utukufu, na sisi ni wadaiwa kwao kutokana na neema kubwa waliyo tupa ya amani na utulivu, isinge patikana neema hii kama sio kujitolea kwao na kumwaga damu zao takatifu”.

Pia kulikua na mashairi kutoka kwa washairi maarufu kama vile dokta Aaid Hariziy na Hussein Ali Rahif pamoja na kaswida kutoka kwa mwanafunzi Ahmad Rashid na Rarul Baaqir, hafla ilihitimishwa kwa kuwapa zawadi wanafamilia wa mashahidi.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha andaa ratiba maalumu ya kutoa zawadi kwa familia za mashahidi toka ilipo tolewa fatwa tukufu ya jihadi ya kujilinda hadi leo, na wamesha saidia maelfu ya familia, hii inatokana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu, kwa ajili ya kudumisha ushindi katika vita dhidi ya magaidi ya Daesh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: