Mazingira ya huzuni yatawala katika Atabatu Abbasiyya tukufu..

Maoni katika picha
Mazingira ya huzuni yametawala katika Atabatu Abbasiyya kutokana na kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa imamu Jafari Swadiq (a.s), kumbukumbu inayo waumiza Ahlulbait na wafuasi wao ya tukio la (25 Shawwal 148h), Mansour Abbasi alipo mpa sumu mwakilishi wake wa Madina bwana Muhammad bun Salmaan naye akamuwekea imamu sumu hiyo katika chakula ikawa ndio sababu ya kifo chake.

Kwa mnasaba huu, hali ya Ataba tukufu ni sawa na Ataba zingine pamoja na mazaru, hufanya taazia za kukumbuka kuuawa kwa maimamu (a.s), mazingira ya huzuni yametawala katika Atabatu Abbasiyya tukufu na zimepandishwa bendera nyeusi katika vibambaza vya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), huku kuta za ndani na nje zikiwa zimewekwa mapambo meusi na taa nyekundu.

Atabatu Abbasiyya kama kawaida yake katika kila mwaka, imeandaa ratiba ya maombolezo yenye vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na kutolewa kwa mihadhara ya kidini na kufanya vikao maalumu vya kuomboleza msiba huu, pia wamejiandaa kupokea vikundi vya waombolezaji kutoka ndani na nje ya mji mtukufu wa Karbala, wanaokuja kutoa mkono wa pole kwa imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: