Kwa picha: Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wasafisha kubba takatifu..

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kulinda muonekano mzuri wa kubba la kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) na kulinda vifuniko vyake vya dhahabu, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kitengo cha uangalizi wa haram tukufu wameanza kazi ya kusafisha kubba tukufu ambayo hufanyika kila wakati kutokana na mazingira ya hali ya hewa katika mji wa Karbala ambayo huathiri muonekano wake.

Kazi ya kusafisha kubba tukufu ambalo mzunguko wake wa nje unaupana wa (mt: 46.5) na sehemu ya juu ina (mt:15) huchukua muda wa siku tano, ambapo uligawa kubba sehemu tano; kila siku husafishwa sehemu moja, kwa kutumia vifaa maalumu na maji pamoja na kitambaa cha koton, kwa ajili ya kukaushia vifuniko vya dhahabu, kwa sababu visopo kaushwa hupelekea kuharibika muonekano wake, kazi hii inahitaji kusoma mazingira ya nyakati na uharaka katika kusafisha, kwa sababu vifuniko vya dhahabu vimegundishwa kwa madini ya chokaa ambayo huathirika haraka kwa maji.

Hatua ya kwanza ya usafishaji wa kubba tukufu imeanzia upande wa mashariki wa mlango wa Furat (Alqamiy), mkabala na saa kwa kuanzia juu kwenda chini, yaani kuanzia sehemu ya bendera tukufu hadi katika kitako cha kubba, baada yake watafuatia kusafisha minara.

Kumbuka kua miaka ya nyuma kazi ya kusafisha kubba ilikua inafanywa na watu kutoka nje ya Ataba tukufu, lakini kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu na baraka za mwenye malalo haya, leo hii kazi hii inafanywa na wataalamu wa ndani ya Ataba tukufu, tena wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi hii kwa kutumia vifaa stahili, na kulifanya kubba tukufu na minara mitakatifu kua katika muonekano mzuri zaidi, muonekano unao endana na utukufu wa mwenye malalo hii takatifu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: