Miongoni mwa ratiba zake endelevu, Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kuwatembelea watu muhimu katika mji mtukufu wa Karbala..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea na ratiba yake ya kuwatembelea watu muhimu wa tabaka tofauti katika mji wa mtukufu wa Karbala, sasa hivi ugeni wa Atabatu Abbasiyya umemtembelea kiongozi wa masayyid wa Aali-twa’ama katika mji mtukufu wa Karbala Sayyid (Muhyi Sayyid Mustwafa Aali-twa’ama) naye ni miongoni mwa watu mashuhuri katika mji wa Karbala na anahistoria ndefu ya kumtumikia imamu Hussein (a.s), pia ni kiongozi wa masayyid wa ukoo wa Twa’ama, alizaliwa (01 Julai 1955m) katika mji wa Karbala, katika familia maarufu ya ma-alawwiy wanaojulikana kwa jina la masayyid wa ukoo wa Twa’ama wanaotokana na kabila ya Aali-faaiz la Ma-alawwiy, nao ni miongoni mwa makabila ya mwanzo kabisa kuishi katika aridhi ya Karbala katikati ya karne ya tatu hijiriyya, naye ni mkuu wa shule ya msingi Sharifu Ridha ya wavulana katika mji mtukufu wa Karbala, vilevile ni muanzilishi wa maombolezo ya watumishi wa kisayyid baada ya kuanguka utawala uliopita.

Wakati akizungumza na wageni alisema kua: “Sio jambo geni wala jipya; mawasiliano haya mnayo fanya Atabatu Abbasiyya tukufu, mimi ninafuraha sana kwa ujio wenu, tumeona namna mnavyo tilia umuhimu wa kuwatembelea watu mashuhuri wa Karbala na familia za mashahidi kutokana na maelekezo ya Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmad Swafi (d.i), tunaishukuru sana Atabatu Abbasiyya kwa kazi nzuri inayofanya.

Pia mazungumzo yao yaligusa upande wa historia, walizungumzia makabila yaliyo ishi Karbala hapo zamani, pamoja na matukio ya kihistoria katika mji huu, na mashambulizi ya kinyama yaliyo ukabili mji huu mtukufu.

Mwishoni mwa mazungumzo yao ugeni kutoka Ataba ulimpa Sayyid (Muhyi Mustwafa Aali-twa’ama) baadhi ya zawadi za kutabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na wakamuombea maisha marefu yenye afya njema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: