Atabatu Abbasiyya tukufu yatoa rambirambi kwa mmoja wa mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji aliye pata shahada katika vita ya kukomboa mji wa Mosul..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu yatoa rambirambi kwa jemedari wake (Abbasi Ali Abdusalmaan) mmoja wa wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) aliye pata shahada wakati akitekeleza wajibu wake wa kitaifa mtukufu katika ukombozi wa Mosul, yeye pamoja na wenzake walipambana na kundi la magaidi waliotaka kuvamia eneo walipokua viongozi wa kikosi katika mji wa Hadhar, ifuatayo ni nakala ya rambirambi:

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu (Wala kabisa msidhanie walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni maiti. bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa mola wao mlezi). Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa pole kwa shahidi wake miongoni mwa mashahidi wa fatwa ya jihadi kifai ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu ambaye ni miongoni mwa wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) aliye pata shahada akiwa anatekeleza jukumu tukufu katika vita ya Mosul, tunamuombo Mola amkutanishe na mashahidi wa Ashura walio pata shahada pamoja na bwana wa mashahidi Abuu Abdilahi Hussein (a.s), na aipe subira familia yake na atunusuru na adui wetu hakika yeye ni msikivu wa dua”.

Alishindikizwa na msafara mkubwa sana, kwanza alifanyiwa ziara na swala kwa niaba katika haram ya imamu Hussein (a.s) kisha mwili wake ukapelekwa katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) akafanyiwa ziara kwa niaba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: