Jarida la Riyadhu Zaharaa (a.s) lafanya kongamano la pili na latangaza washindi wa shindano la utafiti wa wanahabari..

Maoni katika picha
Idara ya wanawake kupitia jarida la Riyadhu Zaharaa (a.s) chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kongamano la pili la wanahabari katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s) ndani ya Ataba tukufu.

Kongamano hili linafanyika sambamba na kumbukumbu ya kutimiza miaka kumi na moja toka kuanzishwa kwa jarida hilo, kongamano lilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ukafuatia wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu, halafu kiongozi wa idara ya wanawake akatoa tamko la makaribisho, kisha mkuu wa wahariri wa jarida la Riyadhu Zaharaa (a.s) akahutubia, katika maelezo yake akasisitiza kuhusu umuhimu wa wanahabari wa kike, halafu likafuata igizo lililo pewa jina la (Wao na Riyadhu) lililo husu Jarida la Riyadhu Zaharaa (a.s).

Baada ya hapo yakatangazwa majina ya washindi wa shindano la wana habari wa kike lililo fanyika mwaka jana. Washindi walikua kama wafuatao:

Mshindi wa kwanza: Khadija Hassan Ali Qasweer kutoka katika mkoa wa Najafu. Utafiti wake ulihusu (Umuhimu wa uthibitisho wa vyombo vya habari katika kulinda historia isipotoshwe).

Mshindi wa pili: Hanaa Baaqir Kamar Khafaji kutoka katika mkoa wa Dhiqaar. Utafiti wake ulihusu (Mtazamo wa vyombo vya habari katika kutangaza mambo ya wanawake).

Mshindi wa tatu: Rasha Abduljabbaar Nasoro kutoka katika mkoa wa Basra. Utafiti wake ulihusu (Sifa za mwana habari wa kiislamu mwenye maadili).

Baada ya hapo wakaingia katika kipengele cha kujadili mihtasari ya tafiti tano, kipengele hicho kiliongozwa na Ustadhat Ruaiy Ali Hussein mkuu wa Redio. Ambazo ni tafiti za:

Ustadhat Khadija Hassan Ali Qasweer kutoka katika mkoa wa Najafu.

Ustadhat Hanaa Baaqir Kamar Khafaji kutoka katika mkoa wa Dhiqaar.

Ustadhat Muntaha Muhsin Muhammad kutoka katika mkoa wa Bagdad.

Ustadhat Kafaah Hadaad kutoka katika mkoa wa Waasit.

Ustadhat Zainabu Hameed Nasraawiy kutoka katika mkoa wa Karbala.

Kumbuka kua kongamano hili linakusudia kutambulisha umuhimu na harakati za wana habari zinazo fanywa na ofisi ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kutambulisha machapisho yake, yakiongozwa na jarida la Riyadhu Zahara (a.s) linalo andika habari za mwanamke na familia ya kiislamu na mambo yanayo husiana nao, ya kimalezi na kimaadili.

Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea toghuti hii: https://alkafeel.net/reyadalzahra
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: